JE UNAJUA KWAMBA WACHAGGA WALIKUWA NA LUGHA YA MAANDISHI?

JE UNAJUA KWAMBA WACHAGGA WALIKUWA NA LUGHA YA MAANDISHI?

Wachagga, Kama Yalivyo Mataifa Mengine Mbalimbali Duniani Kama Wachina, Wagiriki, Waarabu, Warusi, Wakorea n.k., Waliendeleza Lugha Ya Maandishi Kabla Mzungu Yeyote Hajaifahamu Kilimanjaro. Uchaggani Kulikuwa na Shule ya Jadi Ambayo Sio Rasmi Lakini Ilikuwa Ni Lazima Kila Kijana Apitie Akifika Umri Fulani Kupata Mafundisho Maalum Ya Kimaisha Anapoelekea Kuwa Mtu Mzima. Shule Hii Iliitwa MREGHO, na Vijana wa Kichagga Walijifunza Vitu Vingi Vilivyoandikwa Kwa Herufi au Maandishi Ya Kichagga. Walijifunza Kuhusu Siasa za Uchaggani, Kuhusu Sheria Mbalimbali za Vita, Mila, Desturi, Uzazi, Ndoa, Uzalendo n.k., Maandishi Haya Ya Wachagga Yaliandikwa Kwenye Fimbo Maalum Ndefu na Pana.

Maandishi Ya Kichagga, Tofauti na Maandishi Ya Kizungu Yanayotoka Kushoto Kwenda Kulia au Ya Kiarabu Yanayotoka Kulia Kwenda Kushoto, Ya Kichagga Yalisomeka Kutokea Chini Kwenda Juu. Fimbo Hizi Zilizoitwa Fimbo Ya MREGHO, Zilikuwa Kama Ndio Kitabu na Fimbo Moja Ndio Ilikuwa Kama Sura Moja Ya Kitabu. Lugha Ya Maandishi Ya Kichagga Pamoja na Elimu Hii Vilifundishwa na Wazee Maalum Wa Kichagga(Wameeku), Wakishirikiana na Wazazi wa Vijana Husika.

Mmisionari na Mwanazuoni wa Tamaduni za Kichagga, Mjerumani Dr. Bruno Guttman Alijifunza Lugha Hii Ya Maandishi Ya Wachagga Katika Tafiti Zake za Mambo Mbalimbali Ya Wachagga na Kufanya Tafsiri Kwenda Lugha Ya Kijerumani Ambapo Alipata Kitabu Cha Kurasa Zaidi Ya 1,000 Cha Tafsiri Hizi za Maandishi Ya Kichagga. Kwa Kuwa Tulitawaliwa na Wakoloni na Kufuata Mifumo Yao na Baada Ya Wakoloni Tulijikuta Tumeingizwa Tanganyika Ambapo Imekuwa Ni Kama Mwendelezo wa Mifumo Iliyoachwa na Wakoloni, Imekuwa Changamoto Kubwa Kwetu Kuendeleza na Kuyaboresha Maandishi Yetu Pamoja na Mambo Mengine Mengi Mazuri Ya Asili Yetu.

Miaka Ya 1980’s Baada Ya Utawala wa Kikomunisti Tanzania, Wasomi na Wanazuoni wa Kichagga Walijaribu Kuanzisha Vuguvugu La Kurudisha Mafundisho Haya Ya MREGHO Pamoja na Maandishi Haya Ya Kichagga, Japo Haieleweki Walifikia Wapi. Nimeambatanisha Maandishi Ya Mataifa Mengine.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *