UKOO WA MAKERE.

– Ukoo wa Makere ni ukoo wa wachagga unaopatikana zaidi katika kijiji cha Sonu na Ngira, Masama au Machame ya magharibi. Ukoo wa Makere unasemekana kuwa ni tawi la ukoo wa Mboro lililoweka makazi yake ya mwanzoni katika kijiji cha Ngira na Sonu.

– Kutoka kwenye historia inasemekana kwamba tawi hili la ukoo wa Makere lililotokana na ukoo mkubwa wa Mboro walihamia katika eneo la kijiji cha Sonu, Masama baada ya kuvuka mto Marire wakitokea eneo la katikati ya Machame lenye vijiji vya Shari/Uraa, Uswaa na Kyeeri mwanzoni mwa miaka ya 1800. Wakiongozwa na Mzee wa ukoo aliyejulikana kwa jina la Mateba walivuka mto Marire na kuhamishia makazi yao ya kudumu katika kijiji cha Sonu au Ngira, Masama.

– Mzee wa ukoo huu wa Makere ambao unasemekana kuwa ni tawi la ukoo wa Mboro aliyekuwa anafahamika zaidi mpaka katikati ya karne ya 20 alijulikana kwa jina la Lotimsami. Tawi hili la ukoo wa Makere sio tawi lenye watu wengi sana na linalojulikana kwa kiasi kikubwa sana lakini linatokana na ukoo mkubwa sana wenye watu wengi mashuhuri.

– Ukoo wa Makere unapatikana pia kwa kiasi katika vijiji vingine vya karibu na maeneo ya Masama kati pamoja na maeneo ya upande wa magharibi wa mto Marire. Hata hivyo bado tunahitaji taarifa nyingi zaidi na za ndani sana kuhusiana na tawi hili la ukoo mkongwe na mashuhuri wa Makere. Kama kuna chochote unachojua tunahimiza sana kutushirikisha na sisi hapa kwani inasaidia sana kuongeza uelewa na kukuza sana maudhui ya maktaba yetu kwa faida ya sasa na matumizi ya baadaye.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Makere?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Makere?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Makere?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Makere una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Makere wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Makere kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Makere?

7. Wanawake wa ukoo wa Makere huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Makere?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Makere?

Karibu kwa Maoni na Maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *