UKOO WA KULAYA.

– Ukoo wa Kulaya ni kati ya koo kongwe sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Kulaya ni kati ya watu wa mwanzoni zaidi kuweka makazi ya kudumu katika eneo la himaya ya umangi Kibosho.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Kulaya ndio unatajwa kuwa wachagga wa kwanza kufungua soko la kwanza Kibosho kwenye karne ya 17. Mtoto wa Mzee Kulaya aliyejulikana kwa jina la Mono-o-Ruwa ndiye mchagga wa kwanza kufungua soko Kibosho katika eneo la Nchona katika kijiji cha Uchau Kusini, Kibosho.

– Soko hili la Nchona lililopo katika kijiji cha Uchau Kusini Kibosho ambalo lilifunguliwa na Mono-o-Ruwa wa ukoo wa Kulaya takriban miaka 350 mpaka 400 iliyopita bado lipo mpaka leo katika kitongoji cha Nchona kijiji cha Uchau Kusini, Kibosho. Kwa mujibu wa wachagga wenyewe wakazi wa kijiji cha Uchau Kusini ni kwamba soko hili lilikuwa bado linatumika mpaka kwenye miaka ya mwishoni ya 1990’s lakini kwa sasa ni kama limekufa.

– Hata hivyo habari njema ni kwamba juhudi za kulifufua tena soko hili la Nchona lenye historia kubwa zimepamba moto kwani eneo lenyewe la soko la Nchona bado liko wazi na halimilikiwi na mtu. Ukoo wa Kulaya pia ndio wachagga wa mwanzoni waliokuwa karibu na mtawala wa mwanzoni zaidi Kibosho aliyeitwa Yansanya wa kutokea kwenye ukoo Mushi kwani hata eneo la mikutano na ibada takatifu za ukoo wa Mushi Kibosho lipo katika eneo hili hili na Nchona, Uchau Kusini ambapo sio mbali sana na soko lenyewe la kihistoria Kibosho.

– Ukoo wa Kulaya licha ya ukongwe wake ukiwa ni kati ya wachagga wanaotajwa na historia kuwa ni wachagga wa mwanzoni kabisa Kibosho sambamba na Msele na Massawe lakini Wako-Kulaya ambao walikuwa ni watawala wa kijiji cha Uchau Kusini hapo kabla hawakufanikiwa kusambaa eneo kubwa sana. Hata hivyo wachagga wa ukoo wa Kulaya wamefanikiwa kuendelea kuweka ngome yao katika kijiji cha Uchau Kusini hususan katika vitongoji vya Nchona na Nkola, pamoja na kusambaa kwenye vijiji vingine vya Kibosho kwa kiasi.

– Hivyo ukoo wa Kulaya unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Uchau Kusini, Kibosho.

– Ukoo wa Kulaya unapatikana katika kijiji cha Uchau Kaskazini, Kibosho.

– Ukoo wa Kulaya unapatikana katika kijiji cha Otaruni, Kibosho.

– Ukoo wa Kulaya unapatikana katika kijiji cha Maua, Kibosho.

– Ukoo wa Kulaya unapatikana katika kijiji cha Kirima Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Kulaya unapatikana katika kijiji cha Kirima Kati Kibosho.

– Ukoo wa Kulaya unapatikana katika kijiji cha Boro, Kibosho.

– Ukoo wa Kulaya unapatikana katika kijiji cha Kitandu, Kibosho.

– Ukoo wa Kulaya unapatikana katika kijiji cha Mloe, Kibosho.

Mpaka kufikia katikati ya karne ya 20 Mzee kiongozi wa ukoo wa Kulaya aliyekuwa mashuhuri sana aliitwa Leyaro. Hata hivyo bado kuna uhaba mkubwa wa taarifa juu ya ukoo wa Kulaya ambao ni moja kati ya koo zilizokuwa zinaheshimika sana Kibosho kutokana na ukongwe wake, hivyo tunahitaji mchango wa mawazo juu ya taarifa zaidi kuhusu ukoo huu. Taarifa hizi zinasaidia kuongeza katika utafiti na kuongeza wingi wa maudhui ya ukoo huu na koo za wachagga kwa ujumla ili kuweza kutumika katika kuhamasisha wachagga wa ukoo husika kuelekea kufanya mambo makubwa kwa ngazi ya ukoo na ngazi ya mtu mmoja mmoja.

Karibu kwa mchango zaidi wa mawazo.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kulaya?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kulaya?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kulaya?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kulaya una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kulaya wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kulaya kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kulaya?

9. Wanawake wa ukoo wa Kulaya huitwaje?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kulaya?

11. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kulaya?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na ukoo wa Kulaya?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kulaya kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *