UKOO WA SARIA.

– Saria ni ukoo wa wachagga unaopatikana kwa wingi maeneo ya mashariki ya karibu au katika ya Uchagga, Kilimanjaro na maeneo ya mwishoni mwa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Saria japo sio ukoo wenye idadi kubwa sana ya watu lakini ni ukoo wenye mchanganyiko wa baadhi ya watu makini wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali za kimaisha katika taaluma na ujasiriamali.

– Mbali na kuwa ukoo lakini pia jina linaloendana na jina Saria limekuwa likitumika kama jina maeneo mbalimbali ya Uchagga, Kilimanjaro kwa kuwa lina maana inayovutia pia ya kichagga. Kumekuwa na majina ka Isaria, Elisaria, Elimosaria n.k, ambayo yamekuwa yakitumika kama jina.

– Majina haya yanayoendana na jina la ukoo huu yamekuwa yakipenda na kutumika zaidi maeneo ya Machame kuanzia mashariki ambayo ndio Machame yenyewe lakini zaidi katika Machame ya magharibi maarufu kama Masama. Hata hivyo jina hili limekuwa likipendwa pia na kutumika upande wa mashariki ya Uchagga, Kilimanjaro kuanzia sehemu za Uru, Old Moshi na Vunjo kwa ujumla.

– Ukoo wa Saria ambao chimbuko lake haswa linaweza kuwa ni eneo la katikati ya Uchagga, Kilimanjaro au mashariki ya karibu ya Uchagga, Kilimanjaro uliendelea kusambaa kwenye vijiji kadhaa na unapatikana kwa wingi katika baadhi ya vijiji na kwa uchache katika vijiji vingine.

– Ukoo wa Saria unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Tella, Old Moshi.

– Ukoo wa Saria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Saria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Saria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Saria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimangaro/Shokony, Mwika.

– Ukoo wa Saria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Maring’a, Mwika.

– Ukoo wa Saria unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mawanjeni, Mwika.

Tunaomba msaada wa taarifa zaidi juu ya ukoo wa Saria hususan chimbuko lake na kule unakopatikana. Huu ni moja ya koo zenye watu maeneo tofauti lakini wakipatikana kwa uchache zaidi ukilinganisha na koo nyingine. Lakini bado tunahitaji kuwa na maktaba ya maudhui mengi zaidi ya ukoo huu yatakayosaidia kujenga ari, hamasa na mshikamano kwa ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Saria.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Saria?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Saria?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Saria?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Saria una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Saria wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Saria kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Saria?

9. Wanawake wa ukoo wa Saria huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Saria?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Saria?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Saria?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Saria kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp/Call +255 717 452 790

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *