NGUVU YA MAANDISHI NA SALAMU ZA MEI MOSI.

– Siku moja ilikuwa ni mida ya jioni tulikuwa tunafanya maongezi ya kubadilishana mawazo na rafiki yangu mmoja kuhusu mambo mbalimbali katika maisha. Tuliongea mambo mengi sana kwa kirefu lakini ghafla uelekeo wa mazungumzo ukabadilika tukaanza kujadili kuhusu jamii ya wachagga na mambo yao pamoja na mwenendo wa kule wanakoelekea kwa sasa.

– Rafiki yangu huyu akaniambia lakini pamoja na mambo yote mazuri na yenye kuvutia yaliyopata kutokea jamii ya wachagga inaenda kupotea na kusahaulika kabisa. Mimi nikamuuliza kwa nini unasema hivyo? Akaniambia mwenendo tu wa mambo unaonyesha wazi hicho ndio kinachokwenda kutokea na tayari mambo yameendelea kubadilika sana.

– Basi nikamuuliza kwani unafikiri hakuna chochote kinachoweza kufanyika kuzuia hilo? Akasema hakuna. Nikamwambia hakuna changamoto isiyokuwa na suluhisho. Na sehemu kubwa ya suluhisho kwa utamaduni unaopotea ni kuuweka katika maandishi kwani maandishi yanadumu kwa maelfu na maelfu ya miaka yakiendelea kujenga ushawishi na kuathiri mitazamo na fikra za watu kwenye uelekeo fulani wa mambo. Niliweza kumpa mifano mingi sana katika historia jinsi maandishi yalivyoweza na bado yanaendelea kutunza na kuenzi tamaduni mbalimbali duniani pamoja na kujenga umoja na mshikamano imara usiotikisika unaorithishwa kwa vizazi na vizazi na bado tamaduni hizo zina nguvu kubwa kwa maelfu ya miaka sasa.

– Lakini sasa ili maandishi hayo yaweze kuwa na athari kwenye fikra za wengi yanapaswa kusambaa kwa wingi na kuhifadhiwa katika maeneo mengi tofauti tofauti ili yaweze kupatikana kwa lengo la kujenga hamasa na mshikamano kwa walengwa.

– Kitabu cha Miaka 700 ya Wachagga ni mfano wa Nguvu ya Maandishi inayorudisha matumaini ya kuhakikisha jamii ya wachagga na tamaduni zake vinaendelea kuenziwa na kutunzwa kwa faida ya kizazi cha sasa na vingine vinavyofuata. Hii ndio njia pekee ya kuhakikisha kwamba wazazi wetu wa vizazi vingi vilivyopita bado wanaendelea kukumbukwa na kuenziwa sambamba na zile tamaduni nzuri walizoziendeleza na kuturithishi.

– Sasa ili kuhakikisha kwamba tunaingia kwenye historia ya kuwa moja kati ya jamii kongwe na zisizoweza kupotezwa kiurahisi tuendelee kusaidiana katika kuhifadhi maandishi haya yanayoleta uhakika kwa watoto, wajukuu na vizazi vingine vingi vinavyofuata kwamba utamaduni na utambulisho wetu unaendelea kudumu licha ya mabadiliko mengi na makubwa yanayoendelea kutokea. Maandishi haya ndio yanayokwenda kuimarisha mitazamo na fikra chanya zenye kujenga hamasa, umoja na mshikamano kuelekea kusimamia maono makubwa yanayokuja mbeleni.

– Tunafanikisha hayo kwa kununua kitabu cha, “Miaka 700 Ya Wachagga” ikiwa pia ndio njia sahihi ya kusapoti taasisi hii inayolenga kufanya kila linalowezekana ili kurudisha, kuhifadhi na kuenzi historia na tamaduni za jamii ya wachagga ambazo ndio utambulisho wetu halisi kutoka kwenye vizazi vingi vilivyopita.

Karibu Kwa Pamoja Tupambane Kuikuza Hadhi na Heshima Ya Jamii Ya Wachagga Kwa Manufaa Yetu Sote na Nchi Kwa Ujumla.

– Licha Ya Kwamba Kitabu Cha “Miaka 700 Ya Wachagga” Kimeongezeka Ukubwa na Gharama za Uchapishaji Zimeongezeka Zaidi Lakini Tumejitahidi Gharama Ya Kitabu Hiki Imebaki Ile Ile Ya Mwanzo Ya Tshs 35,000/= Kwa Kuwa Lengo Letu Ni Lile Lile La Kuwafikia Wengi. Kitabu Kimetengenezwa Dar es Salaam Hivyo Kwa Mtu Aliyeko Nje Ya Mkoa Atalipia Gharama Za Kusafirisha.

Kama Una Swali Lolote,

Unaweza Kutuma Ujumbe Kwa Whatsapp,

No. +255 754 584 270.

Kulipia.

CRDB BANK,

Acc. No. 01J2030386900.

Jina: SEBASTIAN DASTAN MOSHI.

MPESA.

No. +255 754 584 270.

Jina: SEBASTIAN MOSHI.

Ukikamilisha Malipo,

Tuma Ujumbe wa Muamala Kwa Whatsapp.

No. +255 754 584 270.

Karibu Sana.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *