– Kwayu ni ukoo wa kichagga unaopatikana kwa wingi katika ukanda wa maeneo ya magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo huu ni mkubwa kiasi na mkongwe pia wenye watu wengi makini ambapo baadhi wanafanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali za kimaisha kuanzia taaluma, biashara na ujasiriamali katika taasisi mbalimbali binafsi na za umma.
– Kuna uwezekano mkubwa kwamba ukoo wa Kwayu ambao uko kwa wingi zaidi katika eneo la Machame mashariki una mahusiano ya kindugu na ukoo wa Kway unaopatikana kwa wingi zaidi Kibosho. Nadharia hii inaongezewa nguvu na utafiti wa kina uliofanywa katika miaka ya 1950’s na mwandishi Mary Kathleen Stahl aliyeandika kitabu cha ‘History of the Chagga People of Kilimanjaro” ambaye amezitaja koo za Massawe na Kway kuwa ni koo za mwanzo kabisa kuweka makazi katika eneo la Lyamungo katika ukanda wa juu.
– Mary Kathleen Stahl anaeleza kwamba ukoo wa Massawe ni ukoo wa mwanzo zaidi kuweka makazi yake katika eneo la Lyamungo ukanda wa juu ambao leo hii katika maeneo ya kijiji cha Lyamungo kati huku ukoo wa Kwai ukiweka makazi yake katika ukanda wa juu zaidi ya ukoo wa Massawe karibu na msitu wa mlima Kilimanjaro ambapo leo hii ni katika kijiji cha Lyamungo Kilanya ambacho ndicho kilichopakana na eneo la msitu wa mlima Kilimanjaro.
– Lakini licha ya Mary Kathleen Stahl kuutaja ukoo wa Kwai kwamba uliweka makazi yake katika eneo ambalo leo ni hii ni kijiji cha Lyamungo Kilanya kilichopo juu kabisa kikipakana na msitu kijiji hiki kinakaliwa kwa wingi zaidi na ukoo wa Kwayu na sio Kwai ambao wanapatikana zaidi maeneo ya Kibosho hasa katika kata ya Kibosho Okaoni. Hivyo kuchanganya huku na ukaribu wa koo hizi hata kijiografia huenda kuna mahusiano ya karibu sana japo watu wengi wa kizazi cha sasa wanaonekana hawaelewi sana kama kuna uhusiano huu.
– Ukoo wa Kwayu umeendelea kusambaa na unapatikana kwa wingi zaidi kwa baadhi ya vijiji na kwa uchache sana katika vijiji vingi lakini katika ukanda huu wa magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro.
– Ukoo wa Kwayu unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Nronga, Machame.
– Ukoo wa Kwayu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Foo, Machame.
– Ukoo wa Kwayu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Wari Sinde, Machame.
– Ukoo wa Kwayu unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Nshara, Machame.
– Ukoo wa Kwayu unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Uduru, Machame.
– Ukoo wa Kwayu unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Nkuu Ndoo, Machame.
– Ukoo wa Kwayu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyamungo Kati, Machame.
– Ukoo wa Kwayu unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Lyamungo-Kilanya, Machame.
Bado kuna sintofahamu kubwa juu ya undani wa ukoo wa Kwayu, hivyo tunahitaji kusikia kutoka kwako nini unachofahamu kuhusiana na ukoo wa Kwayu. Tunahitaji kupata maudhui zaidi kuhusu ukoo wa Kwayu ili kuongezea kwenye maktaba ya ukoo wa Kwayu na kwenye maktaba ya wachagga kwa ujumla. Lengo la kuandika maudhui haya ni ili kujenga umoja na mshikamano dhabiti utakaoongeza hamasa na ari zaidi kwa watu kujiletea maendeleo makubwa kuanzia katika ngazi ya mtu mmoja mmoja na ngazi ya ukoo mzima kwa ujumla. Maudhui yatasaidia pia kuongeza kwenye utafiti unaoendelea na tafiti nyingine zitakazoendelea kufanyika.
Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Kwayu.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kwayu?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kwayu?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kwayu?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kwayu una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Kwayu wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kwayu kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kwayu?
9. Wanawake wa ukoo wa Kwayu huitwaje, na kwa nini?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kwayu?
11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kwayu?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kwayu?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kwayu kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).
urithiwetuwachagga@gmail.com
Whatsapp +255 754 584 270.