“THE JEWISH PHENOMENON”
Hiki Ni Kitabu Kilichoandikwa na Mr. Steven Silbiger, Kinachoelezea Historia, Mapito na Mafanikio Ya Jamii Ya Wayahudi Kwa Kipindi Cha Takriban Miaka 4,000 Mpaka Sasa.
Wayahudi au Waisrael Kwa Mujibu wa Mwandishi Ni Jamii Iliyopitia Nyakati Nyingi Ngumu Katika Kipindi Chote Cha Historia na Wamekuwa Wahanga wa Mateso, Manyanyaso na Mauaji Mengi Ya Kimbari Lakini Wameendelea Kusimama Katika Misingi Yao na Mpaka Leo Ni Jamii Yenye Mafanikio Makubwa Katika Nyanja Mbalimbali za Maisha Hasa Kiuchumi. Mwandishi Steven Silbiger Katika Kitabu Hiki Cha “THE JEWISH PHENOMENON” Anaelezea Njia 7 za Kufanya Utajiri na Mafanikio Ya Jamii Fulani Uendelee Kudumu Kwa Vizazi na Vizazi na Bila Ukuu Wao Kupotea.
Hata Hivyo Kuna Tetesi Nyingi Hasi na Chanya Kuihusu Jamii Hii, Kuna Wanaoamini Ni Jamii Ya Watu Waovu na Wabaya na Kuna Wengine Hasa Baadhi Ya Wakristo Wanaoamini Ni Jamii Takatifu Iliyobarikiwa na Mungu na Hata Kufanya Safari za Mara Kwa Mara Kwenye Nchi Yao Ya Asili Ya Israel Katika Mji Wanaoamini Ni Mtakatifu wa Yerusalemu. Yote Hayo Hayana Maana Sana Kwetu Kikubwa Hapa Sisi Kama Wachagga Tunajaribu Kujifunza Mambo Waliyofanya Ambayo Yameweza Kuwasaidia Kupiga Hatua Kubwa Sana Kiuchumi Katika Viwango Vya Kimataifa na Kumiliki Sehemu Kubwa Ya Uchumi wa Dunia.
Kwa Mujibu wa Mwandishi Bwana Steven Silbiger Sisi Kama Jamii Tunaweza Kujifunza Kutoka Kwa Wayahudi na Kupiga Hatua Kubwa Zaidi Kimaendeleo Katika Uchumi wa Dunia Ya Leo Ambao Umeingia Katika Hatua Ya Utandawazi/Globalization.
Baada Ya Mfululizo wa Makala Ya Kitabu Hiki Cha “THE JEWISH PHENOMENON”, Tutaendelea na Makala za Historia Yetu, Mila na Desturi na Ratiba Nyingine.
Karibuni.
Urithi Wetu Wachagga
urithiwetuwachagga@gmail.com