– (Au Tunafikiri Taasisi Hizi Zilishuka Tu Kutoka Mbinguni?).
1. Picha Na. 1, 2 na 3 Inaonyesha Waasisi Waliojenga Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Kwenye Miaka Ya 1940’s/1950’s Katika Juhudi za Kuleta Maendeleo Makubwa Kwa Jamii Yao. Kikiwa Ndio Taasisi Ya Mwanzoni Kabisa Ya Elimu Ya Juu Tanganyika.
2. Picha Na. 4, 5 na 6 Inaonyesha Baadhi Ya Majengo Ya Chuo Hicho Yakiwa Yameandikwa Majina Ya Watu Waliopewa Heshima Ya Majengo Hayo Kuitwa Kwa Majina Yao Katika Miaka Ya Baadaye.
3. Kwa Namna Hii Ni Rahisi Kuendelea Kuwadharau Watangulizi Wetu/Wazee Wetu na Automatically Kujidharau Sisi Wenyewe Pia Kwa Sababu Sisi Ndio Uzao Wao. Na Badala Yake Kupeleka Heshima Kusikostahili. Hii Pia Ni Namna Inayotumika Kuua Ile Ari Ya Kujiamini na Kuamini Katika Sisi Wenyewe Kufanikisha Mambo Makubwa.
4. Ili Kuweka Rekodi Kwa Usahihi Tuna Wajibu na Jukumu La Kujifunza Historia na Kuendelea Kuirithisha Kwa Vizazi na Vizazi. Hiyo Ndio Namna Bora Ya Kukwepa Upotoshaji Unaobadili Kabisa Mitazamo na Mienendo Yetu na Badala Yake Kujenga Jamii Inayowaza Kwa Usahihi Katika Kulinda Heshima Yao na Utu Wao Kuelekea Kwenye Mafanikio Makubwa.
Una Maoni Gani?
Urithi Wetu Wachagga.
urithiwetuwachagga@gmail.com