UKOO WA MMBANDO.

– Mmbando ni ukoo mkubwa wa wachagga unaopatikana kwa wingi zaidi upande wa mashariki ya kati kuelekea mashariki ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Mmbando ni ukoo wenye watu wengi mashuhuri na wanaofanya vizuri katika biashara, taaluma na hata uongozi.

– Ukoo wa Mmbando umeendelea kusambaa na kuongezekana sana idadi kwenye maeneo mapya walikohamia kutoka kwenye makazi ya mwanzoni. Hata hivyo chimbuko la asili kabisa la ukoo wa Mmbando ndani ya Uchagga, Kilimanjaro bado hatujafanikiwa kulipata.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Leghomulo, Kilema.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Masaera, Kilema.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Rosho, Kilema.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kyou, Kilema.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ruwa, Kilema.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kimaroroni, Kilema.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kiria, Mamba.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kokirie, Mamba.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Mboni, Mamba.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Mmbando unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimangaro, Mwika.

Tunahitaji kupata taarifa zaidi juu ya ukoo wa Mmbando ambao licha ya kuwa na umaarufu kiasi lakini kuna machache sana yanayojulikana kuhusu ukoo huu. Tunahitaji kupata taarifa zaidi za kuongeza kwenye tafiti kuongeza maudhui zaidi ya ukoo huu upate kusomwa zaidi na kufahamika zaidi miongoni mwa jamii ya wachagga.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Mmbando.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mmbando?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mmbando?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mmbando?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mmbando una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Mmbando wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mmbando kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mmbando?

9. Wanawake wa ukoo wa Mmbando huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mmbando?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mmbando?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mmbando?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mmbando kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *