UKOO WA MMASI.

– Mmasi ni ukoo maarufu wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi upande wa magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Mmasi wamesambaa maeneo ya vijiji vingi vya eneo la magharibi ya kati ya Uchagga Kilimanjaro hususan upande wa magharibi katika maeneo zilipokuwepo himaya za umangi Kibosho na Kindi.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Mmasi unaaminika kwamba ni ukoo uliokuwa unatoa wanajeshi hodari na wapiganaji jasiri enzi za tawala za umangi Uchaggani, Kilimanjaro. Ukoo wa umeendelea kutoa watu wengi wanaofanya vizuri katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali, biashara na hata viongozi katika taasisi mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi ambapo baadhi wana mafanikio makubwa.

– Licha ya uwepo wa ukoo huu mkubwa wa Mmasi unaopatikana maeneo ya magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro yaani katika maeneo zilizokuwepo himaya za umangi Kibosho na Kindi lakini pia wapo Mmasi wanaopatikana upande wa magharibi zaidi katika iliyokuwa himaya ya umangi Machame.

– Ukoo huu wa Mmasi unaopatikana magharibi zaidi Machame unafahamika kwamba ni tawi la ukoo wa Nkya sambamba na matawi mengine ya ukoo wa Nkya ya Munisi na Nyari. Hata hivyo bado hatuna taarifa za moja kwa moja zinazothibitisha kama ukoo huu wa Mmasi wa Machame ambalo ni tawi la ukoo wa Nkya endapo una uhusiano na ukoo wa Mmasi unapatikana kwa wingi sana Kibosho hususan upande wa magharibi mpaka katikati.

– Ukoo wa Mmasi ndani ya Kibosho unasemekana umegawanyika katika makundi kama sita hivi, ambapo kuna Mmasi Choo/Sala/Iramba, Mmasi Mdawa, Mmasi Mambo/Masaule, Mmasi Nkolo, Mmasi Lyatuu na Mmasi Mborro. Ukoo wa Mmasi umeendelea kusambaa zaidi na unapatikana katika vijiji vingi vya jirani na chimbuko magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro.

– Hivyo ukoo wa Mmasi unapatikana katika kijiji cha Foo, Machame.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Manushi Sinde, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Manushi Ndoo, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Mkomongo, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Umbwe Sinde, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kindi Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kindi Msasani, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kindi Muyuni, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Sambarai, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mloe, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Sisamaro, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Dakau, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Uri, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Uchau Kaskazini, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Uchau Kusini, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Otaruni, Kibosho.

– Ukoo wa Mmasi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sungu, Kibosho.

Kutokana na kuwa na taarifa tofauti tofauti ni wazi kwamba tunahitaji kufahamu kwa undani zaidi juu ya ukoo huu wa Mmasi uliosambaa zaidi maeneo ya magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro pamoja na magharibi zaidi. Taarifa hizi licha ya kuongeza sana katika tafiti, maudhui na maktaba ya koo za wachagga, Kilimanjaro lakini zinasaidia sana katika kujenga hamasa na mshikamano baina ya wanaukoo na wachagga kwa ujumla. Pia zinalenga kuamsha ari ya umoja na kujitambua kuelekea kufanya makubwa zaidi kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja, ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Mmasi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mmasi?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mmasi?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mmasi?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mmasi una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Mmasi wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mmasi kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mmasi?

9. Wanawake wa ukoo wa Mmasi huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mmasi?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mmasi?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mmasi?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mmasi kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *