KITABU CHA “MIAKA 700 YA WACHAGGA” TOLEO LA 2023.

Umashuhuri wa Jamii Ya Watu Unatokana na Nini?

Wote Tunafahamu Kwamba Kuna Faida Nyingi Sana Zinazotokana na Jamii Ya Watu Kuwa Mashuhuri au Maarufu, Faida Ambazo Zina Manufaa Kwa Watu wa Ile Jamii Husika. Manufaa Hayo ni Pamoja na Kwanza Jamii Husika Kujikubali na Kujiheshimu sana Wenyewe(Self Esteem) na Pia Jamii Husika Kuheshimwa Sana na Watu wa Kutoka Nje Ya Jamii Hiyo. Kuheshimiwa Huku Pamoja na Kwamba Kunaleta Hali Ya Kujisikia Furaha na Fahari Lakini Kuna Baadhi Ya Fursa za Kijamii Zinazoambatana na Umashuhuri Huo.

Sasa Umashuhuri wa Jamii Ya Watu Huchangiwa sana na Hadithi Zinazosikika na Kusomwa Kuhusu Watu wa Jamii Husika. Hadithi Hizo Ili Ziwe Chanya Zinapaswa Kuandikwa Kizalendo na Kwa Upendo wa Hali Ya Juu na Wazalendo wa Jamii Husika. Watu wa Jamii Husika na Wale wa Kutoka Nje Ya Jamii Hiyo Wanaposoma Hadithi Hizo Wanaifahamu Jamii Hiyo na Kuiheshimu Kutokana na Yale Waliyosoma au Kusikia Kuhusu Watu Wake.

Kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” Ni Fursa Kwa Jamii Ya Wachagga Kusambaza Hadithi Zake Kwa Wachagga Wenyewe na Hata Watu Wanaotoka Nje Ya Jamii Ya Wachagga. Kufahamika Kwa Hadithi Za Wachagga na Mambo Yao Ni Hatua Muhimu Ya Kukuza Hadhi na Heshima Ya Jamii Ya Wachagga Miongoni Mwetu Wenyewe na Kwa Wa Nje Ya Jamii Yetu Tunaohusiana Nao Kwa Namna Moja Au Nyingine.

Hivyo Ili Kukuza Hadhi na Heshima Ya Wachagga Tunapaswa Kuhakikisha Kwamba Maudhui Haya Matukufu Ya Mwenendo wa Siasa Za Wachagga Kwa Kipindi Cha Takriban Miaka 700 Yanasambaa na Kufahamika na Watu Wengi wa Kutoka Ndani na Nje ya Jamii Ya Wachagga. Jukumu Hilo ni Letu Sote Kuhakikisha Tunawafikia Watu Wengi Zaidi Kwa Namna Moja au Nyingine Kupitia Kununua na Kutangaza Zaidi kwa Watu Wengi Kitabu Hiki Kilichojumuisha Maudhui Mengi Sana Ya Kihistoria Ya Wachagga.

KITABU CHA “MIAKA 700 YA WACHAGGA” TOLEO LA 2023 Ni Kitabu Kile Kile Cha Miaka 700 Ya Wachagga Lakini Chenye Nyongeza Kiasi Kwa Baadhi Ya Maeneo Ambayo Taarifa Zake Hazikuwa Bayana Sana Hapo Kabla Hususan Katika Himaya za Eneo La Rombo. Pia Kuna Picha Mpya za Baadhi Ya Watawala wa Eneo La Rombo Kama Vile Wamangi wa Kirua Rombo, Mrere na Olele.

Kitabu Hiki Kimesheheni Historia Kubwa Sana Ya Wachagga Iliyojumuishwa Kwa Pamoja Ambayo Haipatikani Kwenye Kitabu Kingine Chochote Kinachojulikana Kwa Pamoja na Iliyohusisha Utafiti wa Tangu Zamani Mpaka Miaka Ya Sasa Hivi.

Kwa Wale Ambao Walikosa Vitabu Kwa Sababu Vilikuwa Vimeisha Sasa Tumeingia Kwenye Awamu Nyingine Ya Toleo Lililoboreshwa Zaidi na Tumeanza Kuuza.

Ofisi Zetu Kwa Dar es Salaam ni Mbezi Beach, Tangi Bovu Opposite na Mbezi Shule, Katika Jengo La Mbezi Beach Lutheran Centre “MBLC” Ghorofa Ya Pili, Wing “A”. Ukifika Ghorofa Ya 2 Basi Moja kwa Moja Umefika Kwenye Ofisi Zetu.

Kwa Wale wa Bagamoyo Road Wanaotokea Mjini Kuelekea Mbezi Beach, Kunduchi, Ununio, Tegeta, Salasala, Mbweni, Bunju Kuelekea Mapinga Pamoja na Goba Unaweza Kupitia Tu Ofisini na Kuondoka na Nakala Zako. Kwa Wengine wa Dar es Salaam Pia Unaweza Kufika Ofisini Kuchukua au Kuletewa Nakala Zako Popote Ulipo na Kulipia Deivery. Kwa Sehemu Nyingine Yoyote Mikoani na Nje Ya Nchi Tunatuma Idadi Yoyote Ya Nakala.

NOTE: Kuna Wanaoomba Kuwekewa Nakala, Halafu Vitabu Vinauzwa Mpaka Vinaisha, Wanapokuja Kupiga Simu na Kukuta Vitabu Viliisha Wanalalamika Kwa Nini Hawakuhifadhiwa. Tunashauri Ili Kuepuka Hili Ni Vyema Ukalipia, Kitabu Chako Hakitauzwa Bali Kitahifadhiwa. Ikiwa Bado Hujalipia Halafu Kitabu Kikauzwa Haipaswi Kuwa Lawama Isipokuwa Kama Umelipia Angalau Nusu Ya Gharama. Pia Tunaomba Radhi Kwa Yule Ambaye Vitabu Vyake Viliuzwa Akiwa Ameshalipia, Viliuzwa Kimakosa na Waliokuwepo Ofisini, Kwa Sasa Vitabu Vyake Vimeshahifadhiwa na Atafikishiwa.

Karibu Kwa Pamoja Tupambane Kuikuza Hadhi na Heshima Ya Jamii Ya Wachagga Kwa Manufaa Yetu Sote na Nchi Kwa Ujumla.

Licha Ya Kwamba Kitabu Cha “Miaka 700 Ya Wachagga” Kimeongezeka Ukubwa na Gharama za Uchapishaji Zimeongezeka Zaidi Lakini Tumejitahidi Gharama Ya Kitabu Hiki Imebaki Ile Ile Ya Mwanzo Ya Tshs 35,000/= Kwa Kuwa Lengo Letu Ni Lile Lile La Kuwafikia Wengi. Kitabu Kimetengenezwa Dar es Salaam Hivyo Kwa Mtu Aliyeko Nje Ya Mkoa Atalipia Gharama Za Kusafirisha.

Kama Una Swali Lolote,

Unaweza Kutuma Ujumbe Kwa Whatsapp,

No. +255 754 584 270.

Kulipia.

CRDB BANK,

Acc. No. 01J2030386900.

Jina: SEBASTIAN DASTAN MOSHI.

MPESA.

No. +255 754 584 270.

Jina: SEBASTIAN MOSHI.

Ukikamilisha Malipo,

Tuma Ujumbe wa Muamala Kwa Whatsapp.

No. +255 754 584 270.

Karibu Sana.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *