UKOO WA LYARUU.

– Lyaruu ni ukoo wa kichagga unaopatikana kwa kiasi katika vijiji vichache vya maeneo ya ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Lyaruu ni ukoo mdogo lakini wenye watu wengi makini wanaofanya vizuri katika tasnia mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi kuanzia kwenye taaluma, biashara na ujasiriamali.

– Kutoka kwenye historia kuna watu wanaamini kwamba kuna uhusiana kati ya ukoo wa Lyaruu na ukoo maarufu zaidi wa Lyatuu unaopatikana kwa wingi zaidi katika vijiji vingi vya Old Moshi na kwa uchache katika baadhi ya vijiji vya Kibosho. Hata hivyo hatujaweza kupata taarifa za kutosha kama kweli kuna uhusiano wa kihistoria kati ya ukoo wa Lyaruu na ukoo wa Lyatuu, hivyo kwa wenye kufahamu kuhusu chimbuko hili wanaweza kutusaidia.

– Ukoo wa Lyaruu umesambaa kwa kiasi katika baadhi ya vijiji vya eneo la mwanzoni na mwishoni mwa ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro.

– Ukoo wa Lyaruu unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kilema chini, Kilema.

– Ukoo wa Lyaruu unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Masaera, Kilema.

– Ukoo wa Lyaruu unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Ngangu, Kilema.

– Ukoo wa Lyaruu unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kimaroroni, Kilema.

Japo ukoo wa Lyaruu sio ukoo uliosambaa sana lakini bado kuna taarifa nyingi kuhusu ukoo huu wenye wa watu makini. Bado hatujaweza kupata taarifa za uhakika zaidi ya tetesi kwamba huenda ukoo wa Lyaruu chimbuko lake ni ukoo wa Lyatuu ambayo inakaribiana sana, hivyo tunahitaji kufahamu zaidi kuhusu ukoo huu wa Lyaruu ili kuongeza maudhui zaidi katika maktaba yake. Tunahitaji kuhakikisha kwamba kuna taarifa za kutosha juu ya ukoo huu kwa watu wake kuweza kujenga umoja na mshikamano na hamasa zaidi katika kujiletea maendeleo makubwa. Ni matumaini yetu kwamba tutapata taarifa zaidi ili kuongeza sana maudhui katika maktaba ya ukoo na wachagga kwa ujumla kuanzia maktaba za mtandaoni na baadaye zile halisia.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Lyaruu.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Lyaruu?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Lyaruu?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Lyaruu?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Lyaruu una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Lyaruu wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Lyaruu kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Lyaruu?

9. Wanawake wa ukoo wa Lyaruu huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Lyaruu?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Lyaruu?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Lyaruu?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Lyaruu kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *