UKOO WA CHAO.

– Chao ni ukoo wa wachagga wanaopatikana zaidi maeneo ya ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Chao sio ukoo mkubwa wala unaopatikana katika vijiji vya maeneo mengi lakini ni ukoo wenye watu wengi makini na wasomi wanaofanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali.

– Kutoka kwenye kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” ukoo wa Chao haujazungumziwa lakini sehemu ya watu wa ukoo huu walijihusisha pia kwa kiasi na kazi za kufua vyuma na utengenezajiwa silaha bora za kivita. Ukoo wa Chao umeendelea kukua na kuongezeka zaidi kutoka katika eneo la asili Kilimanjaro, Mamba kwenda maeneo mengine zaidi.

– Ukoo wa Chao unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimbogho, Mamba.

– Ukoo wa Chao unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Komakundi, Mamba.

– Ukoo wa Chao unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Chao unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Chao unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Msae Kinyamvuo, Mwika.

– Ukoo wa Chao unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Maring’a, Mwika.

Ukoo wa Chao ni ukoo wa kipekee, hata hivyo ni wenye wasomi wengi na watu wanaofanya vizuri sana. Lakini pamoja na hayo bado hakuna maudhui mengi yaliyoandikwa kuhusu ukoo huu, hivyo kuna maswali mengi ambayo hayajajibiki kuhusu ukoo wa Chao. Tunahitaji kufahamu mengi zaidi kuhusu ukoo wa Chao ili kuhifadhi maudhui mengi zaidi katika maktaba ya ukoo huu na jamii ya wachagga kwa ujumla. Tunahitaji kuhifadhi taarifa na maudhui katika maktaba za mitandaoni na maktaba halisi pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja kujitambua na kujijengea kujiamini zaidi kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha katika ngazi ya mtu mmoja mmoja kwenye ukoo wa Chao, ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Chao.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Chao?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Chao?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Chao?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Chao una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Chao wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Chao kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Chao?

9. Wanawake wa ukoo wa Chao huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Chao?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Chao?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Chao?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Chao kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *