UKOO WA MATEMBA.

– Matemba ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi katika eneo la ukanda wa katikati wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Matemba ni ukoo wenye watu wengi makini wanaofanya vizuri sana kitaaluma na katika biashara na ujasiriamali katika taasisi mbalimbali za umma binafsi na hata katika mashirika makubwa.

– Ukoo wa Matemba pia ni ukoo wa watu wenye umoja na mshikamano sana katika mambo yao kuanzia ngazi ya familia mpaka ngazi ya ukoo wenyewe. Hata hivyo licha ya kwamba katika kitabu cha “Miaka 700 ya Wachagga” ukoo huu haujazungumziwa lakini watu wengi na pengine hata ndani ya ukoo wenyewe wanahusianisha ukoo huu wa Matemba kama ukoo na ukoo wa Temba /Teemba uliozungumzwa sana katika kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” na unaopatikana katika maeneo yote ya Uchagga, Kilimanjaro kuanzia magharibi ya mbali Siha na Machame mpaka mashariki ya mbali kabisa Tarakea, Rombo. Hata hivyo ukoo wa Matemba wenyewe unapatikana katika eneo la mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro pekee.

– Hili linachangiwa na ukweli kwamba baadhi ya wachagga wa ukoo wa Matemba kujiita Temba kama jina rasmi la ukoo wa kifupi tu, wakati mwingine kama jina lisilo rasmi.

– Hivyo ukoo wa Matemba unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kokirie, Mamba.

– Ukoo wa Matemba unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mboni, Mamba.

– Ukoo wa Matemba unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Mboni, Kitongoji cha Maande.

Ukoo wa Matemba japo sio ukoo mkubwa lakini ni ukoo wa watu makini na wenye umoja na mshikamano sana wanaofanya vizuri katika maeneo mengi. Huu ni ukoo ambao licha ya kuwa na wasomi wengi pia lakini bado hakuna maudhui mengi yaliyoandikwa kuhusu ukoo huu wenyewe ukiondoa ukoo wa Temba wenyewe unaohusishwa nao, hivyo kuna maswali mengi ambayo hayajajibiki kuhusu ukoo wa Matemba wenyewe kama tawi pengine la ukoo mkubwa. Tunahitaji kufahamu mengi zaidi kuhusu ukoo wa Matemba ili kuhifadhi maudhui mengi zaidi katika maktaba ya ukoo huu na jamii ya wachagga kwa ujumla. Tunahitaji kuhifadhi taarifa na maudhui katika maktaba za mitandaoni na maktaba halisi pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja kujitambua na kujijengea kujiamini zaidi kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha katika ngazi ya mtu mmoja mmoja kwenye ukoo, ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Matemba.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Matemba?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Matemba?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Matemba?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Matemba una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Matemba wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Matemba kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Matemba?

9. Wanawake wa ukoo wa Matemba huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Matemba?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Matemba?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Matemba?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Matemba kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255754584270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *