UKOO WA MAKUNDI.

– Ukoo wa Makundi ni ukoo mashuhuri sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro na wenye sifa ya kipekee sana. Wachagga wa ukoo wa Makundi wamekuwa ni watu wapambanaji siku zote na waliojiwekea viwango vya juu sana katika mengi wanayofanya. Hawa wamekuwa ni watu wanaoamini katika juhudi, umoja na mshikamano kitu ambacho wameweza kuambukiza hata kwa majirani zao wa koo nyingine.

– Kutoka kwenye historia kwa kipindi cha takriban miaka 400 au zaidi ukoo wa Makundi wamekuwa wakisifika katika uhodari na ubunifu mkubwa wa utengenezaji silaha bora za kivita na vyombo vingine vinahusisha ufuaji wa vyuma. Makundi umekuwa ni moja kati ya koo chache zilizoweza kuleta heshima kubwa kwa jamii ya wachagga kwa ubunifu na ukuaji wa teknolojia mpaka kufikia mwanzoni mwa karne ya 20 zilizoweza kushangaza wageni wengi waliotembelea Afrika mashariki hususan wazungu kutoka Ulaya.

– Kutokana na kuweka nguvu, muda na akili zao kwenye kazi ya kufua vyuma na kutengeneza vyombo mbalimbali vya vyuma hususan silaha ukoo wa Makundi haukuwa unatoa askari wa jeshi la kwenda vitani wakati wa vita vya zamani vya wachagga. Jambo hilo lilipelekea ukoo wa Makundi kufanya kazi kubwa na nzuri ya ufuaji wa vyuma na hivyo kuuza silaha hata ndani ya Kilimanjaro kwenyewe ambako sio kila eneo wachagga waliwekeza kwenye utengenezaji mkubwa wa silaha kama ilivyokuwa kwa himaya ya umangi Mamba.

– Mbali na uchapakazi na ubunifu ukoo wa Makundi ambao unapatikana kwa wingi na chimbuko lake katika kijiji cha Komakundi, Mamba wameweza kujitofautisha kwa kuweka bidii kubwa kwenye masomo na kujitahidi kuchangamsha sana eneo lao. Hata hivyo sambamba na koo nyingine za eneo la Mamba ukoo wa Makundi umeongezeka sana idadi na hivyo kusambaa maeneo mengine mengi mashariki na magharibi ya eneo lao la asili Mamba.

– Ukoo wa Makundi sambamba na koo nyingi waliokuwa mahodari wa kufua vyuma waliweza kuuza silaha na vyombo vingine walivyokuwa wanatengeneza kwa jamii nyingine nje ya Kilimanjaro kama vile wamasai na hivyo kunufaika zaidi kiuchumi. Japo ukuaji wa teknolojia ya ufuaji wa vyuma ni kama umedumaa kwa sasa lakini bado mpaka leo baadhi ya wachagga wa ukoo wa Makundi na koo nyingine bado wanaendelea na kazi hiyo. Hata hivyo kuanzia karne ya 20 watu wengi wa ukoo wa Makundi walikuja kuweka bidii kubwa kwenye elimu ya kisasa na hivyo kuboresha zaidi maisha yao kwa viwango vya kisasa.

– Ukoo wa Makundi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mashua, Masama.

– Ukoo wa Makundi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Makundi umesambaa na hivyo unapatikana kwa uchache kwenye baadhi ya vijiji vya Marangu.

– Ukoo wa Makundi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Komakundi, Mamba.

– Ukoo wa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mboni, Mamba.

– Ukoo wa Makundi wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kiria, Mamba.

– Ukoo wa Makundi wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkolowony, Mamba.

– Ukoo wa Makundi wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimbogho, Mamba.

– Ukoo wa Makundi wanapatikana katika kijiji cha Lekura, Mamba.

– Ukoo wa Makundi wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Msae Kinyamvuo, Mwika.

– Ukoo wa Makundi wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Makundi wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Maring’a, Mwika.

– Ukoo wa Makundi wanapatikana katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Makundi wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Makundi wanapatikana kwa kiasi katika vijiji vya kata ya Mahida, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Makundi wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mamsera Juu, Mamsera, Rombo.

Licha ya kwamba ukoo wa Makundi ni ukoo mashuhuri na wenye wasomi wengi wanaofanya vizuri sana maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro, nje ya Tanzania na hata nje ya nchi kwa kiasi kikubwa lakini bado kuna uhaba mkubwa wa taarifa juu ya ukoo huu. Tunahitaji kupata taarifa zaidi kuhusu ukoo wa Makundi ili kusaidia katika utafiti na hata kukuza maudhui zaidi ya ukoo huu wenye heshima ya kipekee yatakayochangia katika kuhamasisha mshikamano zaidi wa kiukoo kuelekea kufanya vizuri zaidi kwa ngazi ya ukoo na kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja wa kutokea ukoo husika.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Makundi?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Makundi?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Makundi?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Makundi una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Makundi wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mariki kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Makundi?

9. Wanawake wa ukoo wa Makundi huitwaje?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Makundi?

11. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Makundi?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na ukoo wa Makundi?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Makundi kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Urithi Wetu Wachagga.

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *