“HATUA MBILI KUBWA MUHIMU, WALIZOKUWA WAMEPIGA WACHAGGA, KABLA YA UKOLONI ZISIZOPEWA UZITO UNAOSTAHILI.”

“HATUA MBILI KUBWA MUHIMU, WALIZOKUWA WAMEPIGA WACHAGGA, KABLA YA UKOLONI ZISIZOPEWA UZITO UNAOSTAHILI.”

1. LUGHA YA MAANDISHI.

2. MAHUSIANO YA KIMATAIFA.

1. LUGHA YA MAANDISHI.

Mabadiliko Ya Kifikra Ya Binadamu(Cognitive Revolution), Yalipelekea Binadamu Wote Kuweza Kugundua Lugha Ya Matamshi Lakini Iliwachukua Binadamu Maelfu Ya Miaka Kuweza Kugundua Lugha Ya Maandishi. Jamii Nyingi Hazikuendeleza Lugha Ya Maandishi na Nyingine Hazikuwa na Maandishi Ya Kujitosheleza.

Wachagga, Kama Yalivyo Baadhi Ya Mataifa Mengine Mbalimbali Duniani Kama Wachina, Wagiriki, Waarabu, Warusi, Wakorea n.k., Waliendeleza Lugha Ya Maandishi Kabla Mzungu Yeyote Hajaifahamu Kilimanjaro.

Uchaggani Kulikuwa na Shule ya Jadi Ambayo Sio Rasmi Lakini Ilikuwa Ni Lazima Kila Kijana Apitie Akifika Umri Fulani Kupata Mafundisho Maalum Ya Kimaisha Anapoelekea Kuwa Mtu Mzima.

Shule Hii Iliitwa MREGHO, na Vijana wa Kichagga Walijifunza Vitu Vingi Vilivyoandikwa Kwa Herufi au Maandishi Ya Kichagga. Walijifunza Kuhusu Siasa za Uchaggani, Kuhusu Sheria Mbalimbali za Vita, Mila, Desturi, Uzazi, Ndoa, Uzalendo n.k.,

Maandishi Haya Ya Wachagga Yaliandikwa Kwenye Fimbo Maalum Ndefu na Pana. Maandishi Ya Kichagga, Tofauti na Maandishi Ya Kizungu Yanayotoka Kushoto Kwenda Kulia au Ya Kiarabu Yanayotoka Kulia Kwenda Kushoto, Ya Kichagga Yalisomeka Kutokea Chini Kwenda Juu.

Fimbo Hizi Zilizoitwa Fimbo Ya MREGHO, Zilikuwa Kama Ndio Kitabu na Fimbo Moja Ndio Ilikuwa Kama Sura Moja Ya Kitabu.

Lugha Ya Maandishi Ya Kichagga Pamoja na Elimu Hii Vilifundishwa na Wazee Maalum Wa Kichagga(Wameeku), Wakishirikiana na Wazazi wa Vijana Husika.

Mmisionari na Mwanazuoni wa Tamaduni za Kichagga, Mjerumani Dr. Bruno Guttman Alijifunza Lugha Hii Ya Maandishi Ya Wachagga Katika Tafiti Zake za Mambo Mbalimbali Ya Wachagga na Kufanya Tafsiri Kwenda Lugha Ya Kijerumani Ambapo Alipata Kitabu Cha Kurasa Zaidi Ya 1,000 Cha Tafsiri Hizi za Maandishi Ya Kichagga.

Kwa Kuwa Tulitawaliwa na Wakoloni na Kufuata Mifumo Yao na Baada Ya Wakoloni Tulijikuta Tumeingizwa Tanganyika Ambapo Imekuwa Ni Kama Mwendelezo wa Mifumo Iliyoachwa na Wakoloni, Imekuwa Changamoto Kubwa Kwetu Kuendeleza na Kuyaboresha Maandishi Yetu Pamoja na Mambo Mengine Mengi Mazuri Ya Asili Yetu.

Miaka Ya 1980’s Baada Ya Utawala wa Kikomunisti Tanzania, Wasomi na Wanazuoni wa Kichagga Walijaribu Kuanzisha Vuguvugu La Kurudisha Mafundisho Haya Ya MREGHO Pamoja na Maandishi Haya Ya Kichagga, Japo Haieleweki Walifikia Wapi.

Hata Hivyo Lugha Ya Maandishi Ya Kichagga Haikuweza Kuhifadhi Mambo Mengi na Hivyo Vitu Kama Historia, Falsafa, Tamaduni na Dini Havikuwekwa Katika Maandishi. Ilibakia Kama Lugha Iliyotumika Kufundishia Baadhi Tu Ya Mambo Katika Maisha Ya Mchagga.

2. MAHUSIANO YA KIMATAIFA.

Kufikia Karne Ya 19 Wachagga Walikuwa Tayari Wana Mahusiano Ya Kidiplomasia na Kibiashara na Nchi Mbalimbali Duniani Zikiwemo Ujerumani, Uingereza, Norway, Ugiriki, Sweden na Hata Kupeleka Mabalozi Ujerumani Kwa Kaiser Wilheln. Watawala wa Uchagga Walikuwa Wakiandikiana Barua, Kutumiana Vifaa Kama Vile Mashine na Hata Kubadilishana Utaalamu. Watawala wa Uchagga Walikuwa Wakipewa Salama Ya Heshima Ya Kupigiwa Mizinga 21 na Ujumbe wa Serikali Ya Uingereza.

Kupitia Mahusiano Haya Tayari Watawala wa Uchagga Walianza Kuhitaji Teknolojia Mbalimbali Zenye Nguvu Zaidi Ambazo Hawakuwa Nazo na Walianza Mikakati Ya Kujenga Shule Kwa Ajili Ya Kuimarisha Zaidi Mahusiano Ya Kidiplomasia na Kukuza Teknolojia Mnamo Karne Ya 19, Kabla Ya Ukoloni.

Hivyo Tayari Kulikuwa na Uhakika Mkubwa wa Kuendelea Kukua na Kuimarika Zaidi Kiuchumi, Kimifumo Ya Utawala na Kiteknolojia Bila Hata Ya Ukoloni Huku Tukitunza na Kuenzi Mambo Mengine Mengi Ya Kwetu Yanayotunza Heshima na Utu Wetu.

#HIZI NI HATUA MBILI KUBWA ZILIZOKUWA ZIMEFIKIWA NA WACHAGGA, KARNE 19 KABLA YA UKOLONI LAKINI ZISIZOPEWA UZITO UNAOSTAHILI#

Karibu kwa maoni.

MJI WA MOSHI ZAMANI BAADA YA RELI KUFIKA
WACHAGGA MIAKA YA 1940’s
WACHAGGA KARNE YA 19 NA KABLA YA HAPO
MJI WA MOSHI MWAKA 2020
WACHAGGA KARNE YA 19 NA KABLA YA HAPO
HOTELI YA KITALII MOSHI MWAKA 2020
WACHAGGA KARNE YA 19

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

  1. Bonaventure Juma Mtei says:

    Ningependa sana kujua zaidi kuhusu lugha ya maandishi ya Wachagga kabla ya ukoloni na elimu ya Wachagga kwa ujumla enzi hizo

    Wataalamu wa historia kuhusu eneo hilo ni kina nani na wapi inapatikana literatura na references.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *