HOSPITALI YA MKOA WA KILIMANJARO, MAWENZI ILIPOTOKEA

#HOSPITALI YA MKOA WA KILIMANJARO, MAWENZI ILIPOTOKEA#.

Kuanzia Karne Ya 19 Mpaka Mwanzoni mwa Karne Ya 20 Mji wa Moshi na Taasisi Zake Vilianzia Old Moshi Katika Kijiji cha Tsudunyi. Taasisi Hizi Zilikuwa ni Pamoja na Ofisi za Utawala Kaskazini Ya Tanganyika, Mahakama, Hospitali, Polisi, Soko, Stesheni n.k.,

Taasisi Hizi Baadaye Mwaka 1919 Zilikuja Kuhama Kutokea Old Moshi, Tsudunyi na Kuhamia Moshi Mjini Ya Sasa Kutokana na Mji Wenyewe wa Moshi Kuhama Kutokea Uchaggani na Kushuka Kwenye Tambarare Ambako Wakati Huo Palikuwa Ni Maporini, Baada Ya Reli Kutokea Pwani Ya Tanga Ilipofika Kwenye Tambarare Hizi za Moshi.

Hospitali Ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi Ni Moja Kati Ya Taasisi Zilizotokea Old Moshi, Tsudunyi Na Kuhamia Moshi Mjini Ilipo Mpaka Leo, Baada Ya Mji Huu Kuhama Kutokea Old Moshi Mwaka 1919, Ambapo Ni Zaidi Ya Miaka 100 Sasa Tangu Mji Huu Umehamia Huku Chini “Mjini”.

Pichani Juu Ni Jengo La Hospitali Ya Mawenzi Wakati Bado Ikiwa Katika Kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi Mwishoni mwa Karne Ya 19.

Picha Ya Chini Ni Moja Kati Ya Mitaa Ya Mji wa Moshi Katika Karne Ya 19 Wakati Huo Bado Mji Upo Old Moshi, Tsudunyi.

Eneo Hili La Old Moshi Kwa Sasa Ndipo Zilipo Ofisi za Halmashauri Ya Wilaya Ya Moshi.

#TULIPOTOKA#

HOSPITALI YA MKOA WA KILIMANJARO, MAWENZI ILIPOTOKEA
HOSPITALI YA MKOA WA KILIMANJARO, MAWENZI ILIPOTOKEA

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *