UTARATIBU WA KUPEWA MAJINA UCHAGGANI.

UTARATIBU WA KUPEWA MAJINA UCHAGGANI.

Kwa Mila na Desturi za Kichagga Kumekuwa na Utaratibu Huu wa Watoto Kupewa Majina Kwa Uchaggani Kote. Utaratibu Huu Kuna Watu Wengine Hawaufahamu Vizuri au Namna Unavyofanya Kazi.

Mila Hii Ya Utoaji Majina Kichagga Huwa Katika Familia Kama Ifuatavyo:

– Mtoto wa Kwanza wa Kiume Hupewa Jina La Baba wa Mume, Ambapo Huitwa Kwa Mazoea Nde-a-mii(Nde ni baba, a ni wa, Mii ni Mume) “Ndeamii” au Kwa Kifupi (Ndamii) Ikimaanisha Baba wa Mume. Huyu ni Baba wa Mume Katika Familia, au Unaweza Kusema Babu Mzaa Baba wa Mtoto. Ambapo Sasa Jina Lake Rasmi Linakuwa Ni Lile Jina Rasmi La Babu Yake Mzaa Baba. Au Ndeamii/Ndamii wa Familia.

– Mtoto wa Pili wa Kiume wa Familia Hupewa Jina La Baba wa Mke Ambapo Huitwa Nde-ya-nka au Nde-ya-mka Ambapo (Nde ni Baba, ya ni wa, Nka au Mka ni Mke), Hivyo Ataitwa Kwa Mazoea Ndeyanka au Ndeyamka. Huyu ni Baba wa Mke Katika Familia au Unaweza Kusema ni Babu Mzaa Mama wa Mtoto. Halafu Jina Lake Rasmi Linakuwa Ni Lile Jina Rasmi La Babu Mzaa Mama wa Mtoto, au Baba wa Mke Katika Familia(Ndeyanka/Ndeyamka).

– Mtoto wa Kwanza wa Kike Katika Familia Hupewa Jina La Mama wa Mume Katika Familia Ambapo Huitwa Kwa Mazoea Ma-mii (Mama wa Mume), Mamii. Huyu ni Mama wa Mume Katika Familia au Unaweza Kusema Bibi Mzaa Baba wa Mtoto. Mamii Huwa Ndio Jina La Mazoea na Jina Lake Rasmi Huwa Ni Lile Jina Rasmi La Mama wa Mume Katika Familia au Bibi Mzaa Baba wa Mtoto.

– Mtoto wa Pili wa Kike Katika Familia Hupewa Jina La Mama wa Mke Ambapo Huitwa Kwa Mazoea Ma-nka au Ma-mka Ambapo Kwa Kuwa “Nka” au “Mka” Ni Mke Humaanisha Mama wa Mke “Manka au Mamka”. Huyu ni Mama wa Mke wa Familia au Tunaweza Kusema ni Bibi Mzaa Mama wa Mtoto. Ambapo “Manka” au “Mamka” Huwa ni Jina Lake La Mazoea na Jina Lake Rasmi Huwa Ni Lile Jina Rasmi La Mama wa Mke wa Familia au Bibi Mzaa Mama wa Mtoto.

– Watoto Wengine Wanaofuata Wa Kiume Huweza Kuitwa Kwa Mazoea Meku, Miku n.k., Na Watoto wa Kike Wanaofuata Huwezi Kuitwa Kyekuwe n.k.,

– Utaratibu Huu Umekuwepo Kwa Miaka Tangu Kale na Kale Uchaggani Kote Japo Miaka Ya Karibuni Umefifia Sana.

– Upande wa Magharibi Ya Uchagga Majina Ya Mazoea Kama Manka, Ndeyanka, Miku, Kyekuwe n.k., Yameendelea Kutumika Sana Mpaka Sasa, Hasa Nyumbani.

Karibu kwa Maoni, Nyongeza, Ushauri n.k.,

WACHAGGA NA MAJINA YA ASILI

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *