MUONEKANO BORA ZAIDI WA KILELE CHA KIBO, MLIMA KILIMANJARO.

MUONEKANO BORA ZAIDI WA KILELE CHA KIBO, MLIMA KILIMANJARO.

Katika Kuizunguka Uchagga, Kilimanjaro Tumeweza Kupata Mwonekano(View) Tofauti Tofauti za Mlima Kilimanjaro kwa Maeneo Mbalimbali.

Muonekano(View) Ya Mlima Kilimanjaro Kwa Ujumla Ni Nzuri Sana Kutokea Kwenye Maeneo Mengi Ya Uchagga Kilimanjaro Kwa Ujumla Lakini Eneo Ambalo Pengine Mlima Unaweza Kuuhisi na Kuuona kwa Ukubwa na Mvuto Zaidi Kuliko Sehemu Nyingine Yoyote ni Ukiwa Kibosho, Hasa Kibosho Kati na Kibosho mashariki.

Ukiwa Kwenye Vijiji Kama Uri, Kirima, Singa, Sungu na Hasa Mweka Ile “The Majestic Kibo Dome”(Kilele cha Kibo) Unakiona Katika Ukubwa na Utukufu Wake Uliotukuka.

Japo Inajulikana Kwamba Jina “Kibosho” Limetokana na Jina La Kichagga “Kiwoso”, Lakini Kulikuwa na Utani Zamani Ambao Sina Uhakika Ulitokea Wapi Kwamba Jina “Kibosho” Limetokana na Neno “Kibo Show” Ikiwa ni Matamshi Ya Mzungu Akiwa Ameiona View Ya Mlima Kilimanjaro Kilele cha Kibo Kutokea Maeneo Hayo Ukiwa Unaonekana Vizuri Sana.

Eneo Lingine Ambalo Unaweza Kuuona Mlima Kilimanjaro Ukiwa Umejitenga na Wenye Mvuto wa Kipekee Japo Hauonekani kwa Karibu Kama Ilivyo Kibosho Ni Ukiwa Katika Eneo La Kiboriloni na Kwa Kiasi Moshi Mjini Pia. Ukiwa Eneo Hili La Kiboriloni Mlima Kilimanjaro Unaonekana Ukiwa Clear na Wenye Mvuto wa Kipekee na Inasemekana Pia Kwamba Asili Ya Neno Kiboriloni ni Matamshi Ya Mzungu “Kibo alone”, Baada Ya Kupata View Ya Mlima Kilimanjaro Kutokea Eneo Hili Yaliyozaa Jina “Kiboriloni”, Hata Hivyo Sina Uhakika na Usemi Huu Ulikoanzia.

Tupe Maoni Yako Kwa Uzoefu Wako Ni Eneo Gani Lingine Unafikiri Lina Muonekano(View) Nzuri Zaidi Ya Mlima Kilimanjaro? Au Unaweza Kutuma Licha Pia.

MUONEKANO WA KILELE CHA KIBO CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA KIBOSHO MWEKA
MUONEKANO WA KILELE CHA KIBO CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA KIBOSHO SINGA CHINI
MUONEKANO WA KILELE CHA KIBO CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA KIBOSHO KIRIMA MASOKA
MUONEKANO WA KILELE CHA KIBO CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA KIBOSHO MWEKA
MUONEKANO WA KILELE CHA KIBO CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA MOSHI MJINI
MUONEKANO WA KILELE CHA KIBO CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA KIBOSHO MWEKA
MUONEKANO WA KILELE CHA KIBO CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA KIBOSHO KIRIMA JUU, MKORING’A
MUONEKANO WA KILELE CHA KIBO CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA KIBOSHO SINGA CHINI
MUONEKANO WA KILELE CHA KIBO CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA KIBOSHO MWEKA
MUONEKANO WA KILELE CHA KIBO CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA MOSHI MJINI

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *