KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO.

KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO.

– Ukizungumzia Mlima Kilimanjaro Watu Wengi Akili Zao Moja kwa Moja Huwa Zinaenda Kwenye Kilele cha Kibo na Kidogo Kilele cha Mawenzi. Kilele cha Shira Watu Wengine Ndio Hawajui Hata Kilipo na Kuna Ambao Hawajui Hata Kama Kipo.

– Kilele cha Mawenzi Kipo Upande wa Mashariki wa Mlima Kilimanjaro na Kinaonekana Vizuri na Kwa Ukubwa Kutokea Rombo, Hasa Ukifika Mashati na Usseri.

– Ukiwa Pale Mrere, Mashati, Rombo au Pale Kingachi, Usseri, Rombo Unaweza Kuiona Mawenzi Vizuri Mpaka Yale Mapengo na Miamba Yake Ilivyochongoka Kwa Usahihi Kabisa.

– Kama Hujawahi Kufika Rombo Hasa Mashati na Usseri, Basi Wewe Mawenzi Bado Huwezi Kusema Unaielewa Vizuri, Kwa Wenzangu wa Kuanzia Vunjo Kuelekea Magharibi Mpaka Siha, Unahitaji Kuitembelea Rombo Ili Kuielewa Mawenzi na Mtu wa Rombo Anaweza Kuikubali Vizuri Kibo Anapokuja Huku Mjini.

– Halafu Sasa Tuna Kilele cha Shira Ambacho Ndio Kilele Kikongwe Zaidi Lakini Hakina Umaarufu, Hiki Unaweza Kukiona Ukiwa Unaelekea Magharibi Uelekeo wa Arusha Mara Baada Ya Kuvuka Mto Kikafu Kuelekea Kwa Sadala na Boma. Kama Hakuna Miti Mirefu Unaweza Kuiona Shira Plateau, Ni Kilele Chenye Tambarare Kubwa.

Tupe Maoni Yako na Mchango Zaidi Eneo Gani Ukikaa Exactly Unapata View Nzuri Zaidi Ya Kilele cha Mawenzi Ndani Ya Rombo?

Kama Kuna Picha Nzuri Pia Tutumie.

KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO.
KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA MRAO, MASHATI, ROMBO
KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO, KUTOKEA KERIO, MASHATI, ROMBO
KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA MRAO, MASHATI, ROMBO
KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO.
KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA KERIO, MASHATI, ROMBO
KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA MRAO, MASHATI, ROMBO
KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA SHULE YA MSINGI KINYAULI, ROMBO
KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA NDUWENI, TARAKEA, ROMBO
KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA NDUWENI, TARAKEA, ROMBO
KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA MBOMAI, TARAKEA, ROMBO
KILELE CHA MAWENZI, CHA MLIMA KILIMANJARO KUTOKEA TARAKEA, ROMBO

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

  1. Mbona machame sijaona jamani?

    1. Machame ipo sana, wewe fanya ku-google utakutana na makala nyingi tu kuihusu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *