MAJINA YA ASILI YA MAENEO YA UCHAGGA, KILIMANJARO

Miaka Mingi Imepita Tangu Tumeanza Kuiacha Asili Yetu Kiasi Kwamba Sisi Wenyewe Tumeendelea Kuwa Ni Wageni kwa Tamaduni Zetu Wenyewe Kadiri Siku Zinavyosonga Mbele.

Mchagga wa Mwaka 1890 Akikutana na Mchagga wa Mwaka 2021 Wakizungumzia Maeneo Ya Kilimanjaro Wanaweza Wasielewane Kabisa Wanachozungumzia.

Leo Tujikumbushe Majina Ya Asili Ya Baadhi Ya Maeneo Ya Uchagga, Kilimanjaro Kabla Hayajabadilika Kutokana na Ujio wa Wageni Ulioyataja Kwa Lafudhi Mbalimbali na Kuyabadili Kabisa na Hata Baadhi Ya Watu wa Leo Hawajui Hata Kama Maeneo Haya Yaliitwa Hivyo Kabla Ya Karne 20 na Haya Yanatumika Sasa ni Mapya Kabisa.

Hata Mpaka Sasa Bado Kuna Wazee Wanayataja Maeneo Haya Kwa Majina Yao Ya Asili Ya Kichagga.

1. Machame Kwa Kichagga Inaitwa MASHAMII.

– Mashami Alikuwa Mmoja Kati Ya Wamangi wa Mwanzo Kabisa wa Machame, Aliyeishi Maeneo Ya Machame Katika Kijiji cha Uswaa Kutoka Ukoo wa Mushi.

2. Kibosho Kwa Kichagga Inaitwa KIWOSOO.

– Kiwoso Alikuwa ni Mmoja Kati Ya Wazee wa Mwanzo Kabisa Kibosho Kutoka Katika Ukoo wa Msele Aliyeishi Katika Kijiji cha Uchau Kitongoji cha Nchona.

3. Uru Kwa Kichagga Inaitwa ORU.

– Oru Maana Yake Ni Uhai.

4. Old Moshi Kwa Kichagga Inaitwa MOCHI.

– Mochi Ilitokana na Kitongoji cha Kimochi Katika Kijiji cha Mowo, Old Moshi. Mochi Ndio Iliyozaa Moshi.

5. Kilema Ilitokana na Neno KYELEMA

– Maana Yake Kilichoshindikana.

6. Marangu Kwa Kichagga Inaitwa MORANG’U.

– Morang’u Maana Yake ni Maji Mengi, Iliitwa Morang’u Kwa Sababu Ni Eneo Lenye Maji Mengi.

7. Mwika Kwa Kichagga Inaitwa MIIKA.

8. Rombo Kwa Kichagga Inaitwa HOROMBO.

– Horombo Alikuwa ni Mangi wa Zamani wa Keni, Rombo Aliyetawala Zaidi Ya Nusu Ya Kilimanjaro Kuanzia Mto Nanga Mpaka Usseri, Rombo. Karibu kwa Nyongeza, Maoni, Swali au Mapendekezo.

UCHAGGANI, KILIMANJARO IMEBADILIKA KWA MENGI SANA

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *