UKOO WA LYATUU.

– Ukoo wa Lyatuu unafahamika kama kati ya koo kongwe zenye chimbuka lake katika eneo la vijiji vya Tsudunyi na Mahoma, Old Moshi. Wachagga wa ukoo wa Lyatuu wanasemekana kwamba walikuwa ni kati ya koo zilizowezesha katika kuimarika kwa taasisi ya umangi katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi.

– Kutoka kwenye historia wachagga wa ukoo wa Lyatuu ambao walitoa watu mashuhuri kama Mzee Imeri Lyatuu wanasemekana kuwa kati ya watu hodari sana kwenye mapambano waliowezesha himaya ya umangi Old Moshi kuwa imara na yenye nguvu sana na iliyofanikiwa kuwa na nguvu kubwa sana sambamba na ushawishi mkubwa Uchaggani, Kilimanjaro. Hii ni kwa sababu ukoo wa Lyatuu ulikuwa na watu hodari, jasiri na wenye akili sana katika vita, mikakati na mapambano.

– Wachagga wa ukoo wa Lyatuu waliendelea kuongezeka idadi na kutanua zaidi matawi yao katika vijiji vingine zaidi vya Uchagga, Kilimanjaro.

– Hivyo ukoo wa Lyatuu unapatikana kwa kiasi katika vijiji vya kata ya Kindi, Kibosho.

– Ukoo wa Lyatuu unapatikana katika kwa wingi kiasi katika kijiji cha Tela, Old Moshi.

– Ukoo wa Lyatuu unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Lyatuu wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi.

– Ukoo wa Lyatuu wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Lyatuu wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Lyatuu wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.

– Ukoo wa Lyatuu wanapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kyou, Kilema.

– Ukoo wa Lyatuu wanapatikana kwa uchache katika kijiji cha Lyasomboro, Marangu.

– Ukoo wa Lyatuu wanapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kimangaro, Mwika.

Hata hivyo licha ya ukoo wa Lyatuu kuwa ni ukoo wenye wasomi wengi lakini bado kuna uhaba mkubwa wa taarifa juu ya ukoo huu, hivyo tunahitaji taarifa zaidi kuhusu ukoo wa Lyatuu ili kuongeza katika utafiti unaoendelea. Taarifa hizi ni muhimu sana pia katika kuongeza maudhui zaidi ya ukoo wa Lyatuu zitakazoweza kuwa chache ya kuhamasisha mshikamano zaidi miongoni mwa wanaukoo huu katika kuelekea kufanya mambo makubwa kwa ngazi ya ukoo na ngazi ya mtu mmoja mmoja wa ukoo wa Lyatuu.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Lyatuu.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Lyatuu?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Lyatuu?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Lyatuu?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Lyatuu una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Lyatuu wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Lyatuu kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Lyatuu?

9. Wanawake wa ukoo wa Lyatuu huitwaje?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Lyatuu?

11. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Lyatuu?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Lyatuu?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Lyatuu kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *