UKOO WA MUSHI/MOSHI.

– Mushi/Moshi ni ukoo mmoja mkubwa sana unaopatikana katika vijiji vingi zaidi Uchaggani, Kilimanjaro pengine kuliko ukoo mwingine wowote wa kichagga ikiwemo ukoo wa Massawe. Kwa mujibu wa takwimu za google kuhusu idadi ya majina ya ukoo, Mushi/Moshi unaonekana ndio ukoo wa kichagga wenye idadi kubwa zaidi ya watu ukipatikana kwa wingi maeneo mengi na kwa uchache baadhi ya maeneo. Moja ya sababu ya wachagga wa ukoo wa Moshi/Mushi kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu ni kwa sababu ndio ukoo ambao ulikuwa unaongoza kwa watu wake kuoa wake wengi na kuzaa watoto wengi kutokana na utajiri mkubwa waliokuwa nao miaka ya zamani.

– Ukoo wa Mushi/Moshi ndio ukoo wa watawala au wamangi, ambapo mtu yeyote anayetokea kwenye kizazi cha mtawala yeyote aliyewahi kukalia kiti cha Umangi Uchaggani kwa miaka iliyopita huitwa kwa ukoo huu. Baadhi ya watu wanaamini kwamba Mushi/Moshi zaidi ya kuwa ukoo ni kama utambulisho wa mwanamfalme prince/princess kwa sababu hiyo ndio tafsiri ya moja kwa moja ya ukoo na japo wachache wamepoteza kumbukumbu lakini mtu yeyote anayeitwa kwa ukoo huu moja kati ya mababu zake alikuwa mtawala/Mangi. Ukoo wa Mushi/Moshi ni ukoo ambao kwa miaka ya zamani walikuwa ni matajiri sana kutokana na nafasi waliyokuwa nayo lakini pia historia inaonyesha kwamba hata uwezo wa kukalia kiti cha utawala na kujiimarisha kwenye utawala yenyewe ilitokana na utajiri mkubwa wa mali waliokuwa nao mwanzoni ulioweza kuwajengea nguvu za ushawishi na nguvu za kijeshi pia.

– Kutoka kwenye historia zamani, kwa sababu mbalimbali lakini muhimu zaidi zikiwa ni za kisiasa familia za wamangi walioana sana wenyewe kwa wenyewe kuimarisha ushirika na undugu na watawla wengi walizingatia sana hilo kwa sababu lilikuja na manufaa makubwa. Ilikuwa ni nadra sana hasa kwa yule mtawala aliyeko madarakani kuoa au kuruhusu binti au kijana wake kuoa au kuolewa na familia isiyo ya utawala. Anaandika mwandishi Mary Kathleen Stahl kwenye kitabu chake cha “Africa’s Dome of Mystery” jambo hili ambalo alilishuhudia wazi kwenye miaka ya 1920’s wakati akiishi Marangu kipindi cha utawala wa Mangi Mlang’a mtoto wa Mangi Ndegoruo Marealle.

– Watawala wengi walikuwa wanaoa kwenye familia nyingine za watawala na wakati mwingine hata kuoana ndugu wa ukoo kwa manufaa ya kisiasa. Mary Kathleen Stahl anasema kwa mfano alikuwa akizungumza na binti mmoja aliyekutana naye Marangu wa kutokea kwenye familia ya Mangi ambaye ndoa yake ilikuwa imevunjika huko Rombo alikokuwa ameolewa kwenye familia ya umangi na amerudi nyumbani lakini akawa amepata mchumba mwingine wa kumuoa hapo hapo Marangu. Lakini kaka yake alikataa kabisa na kumwambia tayari ameshapata posa kutoka kwenye familia ya umangi kutoka huko Sanya Juu na ni lazima aende kuolewa huko. Hayo yote yalifanyika zaidi kwa manufaa ya kisiasa na miiko iliyokuwepo. Japo wakati mwingine hilo liliwezekana kufanyika kwa familia nyingine yenye nguvu kubwa ya ushawishi hata kama sio familia ya umangi.

– Lakini pia ukifuatilia familia za watawala wengi utakuta wana ndugu Kilimanjaro kote sababu ya muunganiko wa familia za wamangi. Kwa mfano licha ya wamangi wa Marangu na Kilema kuwa ni ndugu pia mama yake Mangi Mlang’a wa Marangu aliyeitwa Mamesho ni binti wa Mangi Masaki wa Kilema. Mama yake Mangi Meli wa Old Moshi aliyeitwa Sesembu ni binti wa Mangi Masaki pia wa Kilema. Mama yake Mangi Ngulelo wa Machame ni binti wa Mangi Ndaalio wa Marangu ambaye ni dada yake Mangi Ndegoruo Marealle. Mama yake Mangi Petro Itosi Marealle wa Marangu aliyeitwa Makyaleni ni binti wa Mangi Tengia Ndesserua wa Keni, Rombo. Mangi Ndegoruo Marealle mwenyewe alioa binti wa Mangi Rindi Mandara aliyeitwa Ndasho. Hata Mangi Selengia Kinabo wa Mkuu, Rombo alioa binti wa Mangi Tengia wa Keni, Rombo. Mama yake Mangi Rindi Mandara mwenyewe aliyeitwa Mamchaki ni binti wa Mangi wa Kirua Vunjo aliyeolewa na Mangi Ndetia wa Old Moshi.

– Hiyo ni mifano michache kati ya mingi ambayo imetawala katika historia ya wachagga Kilimanjaro. Hivyo kutokana na ukaribu na kuoana sana ukoo wa watawala ambao pia waliendelea kuoana kwa kuangalia ukaribu wake ndio ulikuwa ukoo wa Mushi/Moshi. Inasemekana kwamba kwa sababu za kisiasa walifika mahali na kuoana hata ndugu. Kama jinsi familia ya Malkia Cleopatra wa Misri ya kale walioana mtu na kaka yake kwa sababu za kisiasa hata Mangi Rongoma wa Kilema inasemekana alioana na dada yake wa damu pia kwa sababu hizo. Mangi Ndegoruo Marealle pia anasemakana alioa ndugu wa karibu kama mtoto wa baba mkubwa au mdogo kwa sababu hizo hizo za kisiasa.

– Kwa matukio hayo pia ambayo yalilenga kupunguza uhasama wa kisiasa na kujenga ushirika Uchaggani ukoo wa Mushi/Moshi uliweza kuimarisha sana nguvu ya ushawishi iliyowasaidia kubaki kwenye kiti cha utawala japo mivutano ya ndani ilikuwa haiishi. Hata hivyo pamoja na kuunganisha ukoo na kuoana zaidi wenyewe kwa wenyewe bado ukoo wa Mushi/Moshi ndio ukoo unaoongoza katika wachagga wote kuwa na uhasama na migogoro ya ndani kwa ndani kuanzia uhasama wa ukoo kati ya himaya moja na nyingine na hata uhasama wa ukoo ndani ya ukoo husika katika himaya hiyo hiyo. Hata mpaka sasa ukitembelea familia za Uchagga utakuta bado kuna migogoro na uhasama zaidi katika koo za watawala kuliko koo nyingine zote.

– Ukoo wa Mushi/Moshi ambao unaaminika na wachagga wa vijiji vingi kwamba ni watu wakorofi na wababe na wasioogopa wala kujali chochote kuna mitazamo mingine iliyokuja na propaganda kwamba ni ukoo wenye “mbaka” ambalo ni neno la kichagga lenye kumaanisha kama ukoo wenye “laana” au “mkosi”. Hii ni kwa sababu kwanza kutokana na kwamba walikuwa ni watawala kuna maeneo mengine ulionekana kufanya uonevu na manyanyaso. Pili ni kwa sababu utawala wowote ni lazima unakusanya kodi ambayo ndio inatumika kwa ajili ya ulinzi, maendeleo na kusaidia pia watawala kujiimarisha kisiasa hivyo kudai kule kodi kulikoambatana na mambo mengine mengi kukajengewa mtazamo hasi sana. Watu wanasema Wamoshi/Wamushi wamekula dhulma za watu kwa kuwa sehemu kubwa ya kodi ilikuwa inadaiwa moja kwa moja tofauti na sasa ambapo serikali nazo zinachukua kodi na kufanya mambo mengi, mengine ya msingi na mengine ya anasa lakini wanajitahidi kuchukua kwa namna ambayo haileti maumivu ya moja kwa moja kama zamani. Ukoo huu pia unaaminika kwamba ulijipendelea sana hasa katika kujigawia ardhi kubwa, nzuri na yenye rutuba zaidi, japo kitu hiki pia kinaonekana kwa watawala dunia nzima ambao hawabanwi na sheria sawa sawa.

– Hata hivyo zaidi mtazamo kwamba ukoo huu una “mbaka” ni umetokana na propaganda zilizoenezwa kubeza taasisi ya umangi Uchaggani ambayo ndio imebeba sehemu kubwa ya historia na ufahari kwa wachagga. Hivyo kubeza au kuipunguzia hadhi taasisi hii moja kwa moja unakuwa umeibeza na kuidharau jamii nzima ya wachagga na utukufu wote iliyojenga kutoka kwenye historia ambao umejumuisha na kuhusisha koo zote za kichagga. Yaani koo zote kwa pamoja na kwa ushirikiano ambao hauwezi kutenguka ndio zimejenga historia yote yenye ufahari mkubwa kwa wachagga. Sehemu kama Kibosho mtazamo huu uko dhahiri kabisa, watu wanasema watu wa ukoo wa kwa Mushi ni hatari na ni kama wamechanganyikiwa.

– Ukoo huu Mushi/Moshi ni ukoo mmoja ambao unatamkwa tofauti kidogo kwa sababu ya lugha ya utamkaji na ambapo upande wa magharibi wa Uchagga kuanzia Siha, Machame, Kibosho na Uru kwa sehemu kubwa wanatumia Mushi wakati Mbokomu, Old Moshi, Kirua Vunjo, Kilema, Marangu, Mamba, Mwika, Keni-Mriti-Mengwe, Mkuu, Mashati na Usseri wanatumia Moshi. Hata hivyo baadhi ya wachagga wa ukoo huu Uru wanatumia Moshi na baadhi ya wachagga wa ukoo huu sehemu za Rombo wanatumia Mushi. Watu mashuhuri wengi katika historia ya wachagga walitokea kwenye ukoo wa Mushi/Moshi na historia zao zinakwenda mpaka takriban miaka 500 iliyopita. Hata hivyo kuna matawi mengi ya ukoo huu ambayo yametokana na watawala maarufu wa zamani ambayo nayo yanatumika kama koo kama vile Shangali, Kisarika, Mandara, Mashingia, Kirita, Kinabo, Marealle, Lemnge, Tengia, Salakana n.k., lakini yote haya yanaangukia kwenye ukoo wa Mushi/Moshi.

– Ukoo wa Mushi/Moshi ambao ndio ukoo wenye matawi mengi zaidi na historia zinazokwenda miaka mingi zaidi iliyopita umeendelea kusambaa kwa wingi na unapatikana karibu kila kijiji mbali na lilipoanzia chimbuko lao ambalo mara nyingi ni kwenye kijiji chenye makazi ya umangi kwa maeneo mengi. Hivyo ukoo huu umesambaa na unapatikana kuanzia magharibi katika kijiji cha Mae, Siha/Sanya Juu.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mashua, Masama.

– Ukoo wa Mushi wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lukani, Masama.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa kiasi Mbwoeera, Masama.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mboreny, Masama.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sonu, Masama.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sawe, Masama.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Mbosho, Masama.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Mroma, Masama.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Lemira, Masama.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Isuki, Masama.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Ng’uni, Masama.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Roo, Masama.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mudio, Masama.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kyeeri, Machame.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Shari/Uraa, Machame.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Uswaa, Machame.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Nronga, Machame.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Foo, Machame.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Wari Ndoo, Machame.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Wari Sinde, Machame.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Uduru, Machame.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Nshara, Machame.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Nkuu, Machame.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi katika vijiji vya kata ya Lyamungo, Machame.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kombo, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkomongo, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Umbwe, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Manushi, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi sana katika vijiji vya Kata ya Kindi, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Otaruni, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Uchau Kusini, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Uchau Kaskazini, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Maua, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Sambarai, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Omarini, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kitandu, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mloe, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Dakau, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Sisamaro, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Uri, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kirima Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kirima Kati, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Boro, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Singa, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sungu, Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mweka Kibosho.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ongoma, Uru.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Okaseni, Uru.

– Ukoo wa Mushi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mawella, Uru.

– Ukoo wa Mushi unapatikana katika kijiji cha Njari, Uru.

– Ukoo wa Mushi unapatikana katika kijiji cha Mrawi, Uru.

– Ukoo wa Mushi unapatikana katika kijiji cha Shimbwe, Uru.

– Ukoo wa Mushi unapatikana katika kijiji cha Mwasi, Uru.

– Ukoo wa Mushi unapatikana katika kijiji cha Mnini, Uru.

– Ukoo wa Moshi unapatikana katika kijiji cha Korini Juu, Mbokomu.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Korini chini, Mbokomu.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Korini Kati, Mbokomu.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Tella, Old Moshi.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Shia, Old Moshi.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Mowo, Old Moshi.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kmare, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana katika kijiji cha Tella, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nduoni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kanji, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Masaera, Kilema.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyura, Kilema.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ngangu, Kilema.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyou, Kilema.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kimaroroni, Kilema.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Rauya, Marangu.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Sembeti, Marangu.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Arisi, Marangu.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mshiri, Marangu.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyasongoro, Marangu.

– Ukoo Moshi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kyala, Marangu.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ashira, Marangu.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kotela, Mamba.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kokirie, Mamba.

– Ukoo Moshi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mkolowony, Mamba.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kimbogho, Mamba.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Lekura, Mamba.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kiria, Mamba.

– Ukoo wa Moshi unapatikana katika kijiji cha Kimangara, Mamba.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mboni, Mamba.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shokony, Mwika.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mengeni chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Aleni chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mengeni Kitasha, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika vijiji vya kata ya Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Makiidi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ibukoni, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijii cha Maharo, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi kidogo katika vijiji vya Kata ya Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kirongo juu, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Samanga, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kingachi, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lesoroma, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kirongo chini, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Leto, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nanjara, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kibaoni, Tarakea Rombo.

– Ukoo Moshi unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mbomai, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Moshi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kikelelwa, Tarakea, Rombo.

Pamoja na kwamba kuna taarifa nyingi sana kwenye vitabu mbalimbali kuhusiana na ukoo wa Mushi/Moshi lakini ukoo huu umeambatana na matata mengi hivyo bado kuna taarifa nyingi zisizojulikana kuhusiana na wachagga wa ukoo wa Mushi/Moshi. Tunahitaji mchango wa mawazo zaidi juu ya ukoo huu ili kuweza kukusanya maudhui ya kutosha kuhusu koo za wachagga na kuhusu ukoo husika.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Mushi/Moshi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mushi/Moshi?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mushi/Moshi?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mushi/Moshi?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mushi/Moshi una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Mushi/Moshi wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mushi/Moshi kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mushi/Moshi?

9. Wanawake wa ukoo wa Mushi/Moshi huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mushi/Moshi?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mushi/Moshi?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mushi/Moshi?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mushi/Moshi kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *