UKOO WA NDOSI.

– Ukoo wa Ndosi ni ukoo mkongwe sana na unaopatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mbweera, Masama kati. Ukoo wa Ndosi ni tawi la ukoo wa Mboro ambao tulishaujadili hapa kwa kina na matawi yake lakini tawi lilikuwa na nguvu sana katika eneo hili la Masama kati na ndio ulikuwa ukoo wa watawala eneo …

UKOO WA NG’UNDA.

– Ukoo wa Ng’unda ni ukoo wa wachagga unaopatikana katika vijiji vya Masama Magharibi kama vile Ng’uni. Huu ni ukoo ambao sio mkubwa sana lakini una watu wengi makini unaoweza kukutana nao katika maeneo mbalimbali. – Hakuna taarifa za kutosha sana kujua chanzo chake halisi au kama huenda ni tawi la ukoo mwingine mkubwa zaidi …

UKOO WA MOSI.

– Ukoo wa Mosi ni ukoo unaopatikana katika himaya ya umangi Siha/Sanya Juu. Hakuna taarifa nyingi juu ya chimbuko la ukoo huu wala uelewa zaidi kama laba ni tawi la ukoo mwingine mkubwa unaojulikana zaidi. – Hata hivyo ukoo wa Mosi ni ukoo wa watu makini na wapambanaji pia. Tumekutana na watu kadhaa wenye uwezo …

UKOO WA KIRUNDWA.

– Ukoo wa Kirundwa au wakati mwingine huitwa Kihundwa ni ukoo mdogo unaopatikana kwa wingi zaidi katika kijiji cha Mese, Siha/Sanya Juu. Ukoo wa Kirundwa unapatikana pia kwa uchache katika vijiji vingine vya Siha/Sanya Juu. – Kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi inasemekana kwamba ukoo wa Kirundwa huenda ni tawi la ukoo wa Munuo wenye …