UKOO WA KAALE.

– Kaale ni ukoo wa wachagga wanaopatikana katika maeneo ya mwishoni mwa ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Kaale sio ukoo mkubwa wala unaopatikana maeneo mengi lakini ni ukoo wa watu makini wanaofanya vizuri sana kitaaluma na kwenye biashara na ujasiriamali.

– Wako wachagga wengi wa ukoo wa Kaale wanaofanya vizuri sana katika taasisi mbalimbali za umma na binafsi na hata kwenye mashirika na taasisi za kimataifa. Ukoo huu wa Kaale pia ni ukoo wenye watu kadhaa mashuhuri katika maeneo tofauti. Ukoo wa Kaale ni ukoo uliosambaa zaidi katika eneo dogo la mwishoni mwa ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro.

– Ukoo wa Kaale unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Kaale unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mawanjeni, Mwika.

– Ukoo wa Kaale unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Maring’a, Mwika.

– Ukoo wa Kaale unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

Tunahitaji ufafanuzi zaidi juu ya ukoo wa Kaale.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Kwayu.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kaale?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kaale?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kaale?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kaale una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kaale wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kaale kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kaale?

9. Wanawake wa ukoo wa Kaale huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kaale?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kaale?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kaale?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kaale kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *