UKOO WA KIMEI.

– Kimei ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi katika lote la mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Kimei ni ukoo wenye watu makini na wanaofanya vizuri katika maeneo na tasnia mbalimbali tangu zamani sana mpaka sasa. Huu ni ukoo wenye watu wanaopenda kujituma sana na hivyo kupata matokeo makubwa katika yale wanayofanya.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Kimei ni moja kati ya koo mashuhuri zilizosifika na hata sasa kuna watu wanaoendelea kusifika kwa uhodari katika kufua vyuma hasa ukoo wa Kimei unaopatikana katika eneo la himaya ya umangi Mamba. Historia inatuonyesha kwamba ukoo wa Kimei ulikuwa ndio ukoo wenye nguvu sana katika eneo la himaya ya umangi Mamba katika nyakati za karne ya 16.

– Baadaye ukoo wa Moshi kwa ushirikiano na ukoo wa Teri waliweza kuungana na kupambana na ukoo huu wa Kimei mpaka kufanikiwa kuunganisha na kisha kuwaweka chini ya utawala wao ndani ya himaya ya umangi Mamba. Katika mapambano haya baadhi ya wachagga wa ukoo wa Kimei walikimbilia kwenye maeneo mengine ya umangi na kusambaa kwenye vijiji vingine hususan katika eneo la Vunjo.

– Ukoo wa Kimei pia walikuwa ni mahodari sana wa kutengeneza silaha bora za kivita sambamba na koo nyingine kama vile Makundi. Uwezo huo wa kipekee uliweza kuwapa nafasi ya kuwa wenye nguvu sana na wanaotawala sehemu kubwa ya Mamba kabla ya kuangusha na kukubali kukaa chini ya utawala wa umangi Mamba. Na hata mpaka leo hii bado kuna wachagga wa ukoo wa Kimei wanaendelea na fani hii ya ufuaji vyuma katika eneo la Mamba wakiendeleza urithi huu unaojulikana kuwepo kwa zaidi ya miaka 400 leo hii. Ukoo wa Kimei umeendelea kuwa ni ukoo wa watu mashuhuri tangu karne nyingi zilizopita mpaka sasa.

– Wachagga wa ukoo wa Kimei wameedelea kusambaa na wanapatikana kwenye maeneo ya vijiji mbalimbali vya Uchagga, Kilimanjaro hususan katika eneo la mashariki ya kati ya Uchagga.

– Ukoo wa Kimei unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kimei unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mmbahe, Marangu.

– Ukoo wa Kimei unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kimbogho, Mamba.

– Ukoo wa Kimei unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mkolowony, Mamba.

– Ukoo wa Kimei unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mrieny, Mamba.

– Ukoo wa Kimei unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kokirie, Mamba.

– Ukoo wa Kimei unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Komakundi, Mamba.

– Ukoo wa Kimei unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mboni, Mamba.

– Ukoo wa Kimei unapatikana wa uchache maeneo ya Mwika Kusini.

Karibu uongeze maudhui zaidi kuhusu ukoo wa Kimei ambao una historia kubwa na ya miaka mingi na karne nyingi katika nchi ya Uchagga, Kilimanjaro. Tunahitaji kuwa na taarifa nyingi sana juu ya ukoo huu mkongwe ili kuongeza katika maktaba ya ukoo na katika maktaba ya jamii ya wachagga kwa ujumla. Maudhui haya yanalenga kujenga hamasa zaidi sambamba na umoja mshikamano kuelekea kufanya makubwa zaidi kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa nzima kwa ujumla.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Kwayu.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kimei?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kimei?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kimei?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kimei una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kimei wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kimei kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kimei?

9. Wanawake wa ukoo wa Kimei huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kimei?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kimei?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kimei?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kimei kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *