UKOO WA OLOTU.

– Ukoo wa Olotu/Ulotu ni tawi la ukoo wa Mallya lenye chimbuko lake katika kijiji cha Sisamaro, Kibosho katika eneo lenye umaarufu zaidi kama Kibosho Maro. Zamani wakijulikana zaidi kama ukoo wa Olotu Mallya hawa ni wachagga wenye ujasiri mkubwa sana katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika maisha ni kati ya koo za wachagga zenye …

UKOO WA MALLYA.

– Ukoo wa Mallya ni ukoo mkubwa mashuhuri na maarufu sana Uchaggani kwa ujumla. Huu ni ukoo unaohusishwa na watu wengi wenye ujasiri mkubwa katika kukabiliana na mambo mbalimbali katika maisha kwa ujumla. – Kutoka kwenye historia ukoo wa Mallya kwa Uchaggani, Kilimanjaro unaonekana kuwa na chimbuko lake katika vijiji vya ukanda wa juu Kibosho …

UKOO WA MSELE.

– Ukoo ni ukoo mkubwa na maarufu sana Kibosho na unasemekana kuwa ndio ukoo mkongwe zaidi Kibosho kwa kupitia kuhesabu vizazi. Inasemekana kwamba mwanzoni ukoo wa Msele walikuwa wanaishi katika ukanda wa juu wa kijiji cha Uri, Kibosho ambapo kwa sasa ni eneo la msitu wa mlima Kilimanjaro kabla ya kushuka na kuweka makazi ya …

UKOO WA KULAYA.

– Ukoo wa Kulaya ni kati ya koo kongwe sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Kulaya ni kati ya watu wa mwanzoni zaidi kuweka makazi ya kudumu katika eneo la himaya ya umangi Kibosho. – Kutoka kwenye historia ukoo wa Kulaya ndio unatajwa kuwa wachagga wa kwanza kufungua soko la kwanza …

UKOO WA MARIKI.

– Ukoo wa Mariki ni ukoo mkongwe sana wa kichagga na maarufu zaidi upande wa mashariki na kati ya Kilimanjaro. Huu ni ukoo uliotoa watu kadhaa mashuhuri ambao wamekuwa na umuhimu mkubwa katika historia ya wachagga Kilimanjaro kama vile Mzee Makiponyi Mariki aliyekuwa baba mlezi wa Mangi Ndegoruo Marealle baada ya kumuoa mama yake aliyeitwa …

UKOO WA LYIMO.

– Ukoo wa Lyimo ni moja ya koo kubwa, kongwe, mashuhuri na maarufu sana unaosambaa maeneo mengi ya Uchaggani, Kilimanjaro na unaopatikana kwa wingi sana kila eneo ulipo. Bila mashaka yoyote huu ni ukoo uliotoa wa wenye wachagga mashuhuri na uliotoa watu wengi sana maarufu katika historia ya wachagga Kilimanjaro kwa karne nyingi zilizopita na …

UKOO WA MACHA.

– Ukoo wa Macha ni ukoo mkubwa wenye idadi kubwa ya watu na uliosambaa maeneo mengi ya uchagga Kilimanjaro. Huu ni ukoo mkongwe na mashuhuri sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro, wenye matawi mengi na unaoweza kuhesabu vizazi vingi vilivyopita. – Kutoka kwenye historia tawi la ukoo wa Macha ambalo ni kongwe zaidi linapatikana katika …

UKOO WA MSHANGA.

– Ukoo wa Mshanga ni ukoo mkongwe na uliotawanyika maeneo mbalimbali ya Uchagga, Kilimanjaro kuanzia magharibi mpaka mashariki kabisa. Huu ni ukoo wa wachagga wasiotajwa sana lakini wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro. Japo ukoo huu unapatikana maeneo mengi lakini karibu kwenye kila eneo wanalopatikana wanapatikana kwa uchache. – Kutoka kwenye …