UKOO WA MLAY.

– Ukoo wa Mlay ni ukoo mkubwa na maarufu sana wa wachagga unaopatikana kwa wingi zaidi upande wa mashariki na kati wa Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu wengi mashuhuri na wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Mlay unasemekana kwamba ndio ukoo mkongwe zaidi katika eneo la Msae lililopo Kaskazini magharibi ya himaya ya umangi Mwika. Hivyo kwa mujibu wa historia eneo la asili la ukoo wa Mlay kwa Kilimanjaro ni Msae, Mwika. Katika eneo hili la Msae ambalo lilikuwa ni himaya ndogo inayojitagemea zamani koo mbili kongwe na zilizowahi kupata umaarufu zikiwa ni Mlay na Mariki, ukoo wa Mlay unasemekana kuwa ndio mkongwe zaidi kuliko hata Mariki yenyewe.

– Tumejifunza kutoka kwenye historia kwamba ukoo wa Mlay uliwahi kutawala eneo hili la Msae, Mwika wakati wa utawala wa Mangi Horombo takriban miaka zaidi ya 200 iliyopita kupitia mtawala aliyeitwa Tenguti ambaye aliteuliwa na Horombo. Baada ya utawala wa Mangi Horombo kuanguka kufuatia kifo chake Tenguti kutokea ukoo huu wa Mlay alijimilikisha mali zote za Mangi Horombo katika eneo hili na hivyo kuendelea kuwa na nguvu ya kutawala Msae. Hata hivyo baadaye baada ya utawala wake kupita na mabadiliko mbalimbali ya kisiasa yaliyoendelea kutokea kutokana na mwenendo wa matukio ya kisiasa ya nyakati tofauti ukoo wa Mariki ulirudi kuwa na nguvu na kukalia tena eneo hili.

– Ukoo wa Mlay uliendelea kusambaa maeneo mengine zaidi ya Kilimanjaro mashariki na magharibi na kuwa unapatikana sehemu nyingi sana na kwa wingi sana pia. Hiyo imepelekea wachagga wa ukoo wa Mlay kuwa ni kati ya wachagga wenye umaarufu sana katika maeneo mengi wanayopatikana ndani na nje ya Kilimanjaro.

– Ukoo wa Mlay unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika Kaskazini.

– Ukoo wa Mlay unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Msae Kinyamvuo Mwika Kaskazini.

– Ukoo wa Mlay unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Lole Marera, Mwika.

– Ukoo wa Mlay unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Lole, Mwika.

– Ukoo wa Mlay unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kondiki, Mwika.

– Ukoo wa Mlay unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Maring’a Mwika.

– Ukoo wa Mlay unapatikana kwa kiasi katika kata ya Mahida na Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Mlay unapatikana katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Mlay unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mrimbo Uuwo, Mwika.

– Ukoo wa Mlay unapatikana katika kijiji cha Kirimeni, Mwika.

– Ukoo wa Mlay unapatikana katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Mlay unapatikana katika baadhi ya vijiji Mamba.

– Ukoo wa Mlay unapatikana katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Mlay unapatikana katika kijiji cha Kyala, Marangu.

– Ukoo wa Mlay unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Shia, Old Moshi.

– Ukoo wa Mlay unapatikana kwa kiasi pia katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Mlay unapatikana kwa wingi kiasi katika kata ya Narumu, Machame.

Ukoo wa Mlay ni mkubwa lakini una taarifa chache ukilinganisha na umashuhuri wake, lakini kwa kuwa una watu wengi tunaamini kuna taarifa nyingi zaidi kuhusiana na ukoo huu kutoka kwa watu mbalimbli hivyo tunahitaji mchango zaidi wa mawazo kuhusu ukoo huu mkubwa na maarufu.

Karibu kwa mchango zaidi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mlay?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mlay?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mlay?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mlay una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Mlay wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mlay kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mlay?

7. Wanawake wa ukoo wa Mlay huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mlay?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mlay?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

  1. Philomena Benedict kitaly Mlay says:

    Umesahau kina Mlay pia tuko Kijiji Cha Shimbi masho Mkuu Rombo
    Mimi ni mjukuu wa Mangi Thomas Mlay..Kwa namba ni mjukuu namba 3

    1. Okay, ahsante sana kunikumbusha hili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *