UKOO WA KIWIA.

– Kiwia ni ukoo wa wachagga uliosambaa katika vijiji kadhaa ndani ya Uchagga hususan maeneo ya katikati ya Uchagga. Japo sio ukoo mkubwa sana lakini wachagga wa ukoo wa Kiwia ni watu wenye kujituma sana na wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Kiwia ulikuwa ni ukoo mashuhuri sana uliokuwa unatawala katika kijiji cha Tela, Old Moshi kwa miaka ya zamani sana ukiwa ndio unatoa watawala wa kijiji hiki. Hata baadaye taasisi ya umangi ilipofikia kuwa na nguvu zaidi ukoo wa Kiwia kutokana na umashuhuri na ushawishi mkubwa uliokuwa nao katika kijiji cha Tela, Old Moshi uliendelea kutoa wachili wa kijiji hiki chini ya taasisi ya umangi.

– Ukoo wa Kiwia umeendelea kukua na kuimarika zaidi, ukiongezeka idadi na kusambaa katika vijiji vingine mbalimbali ndani na nje ya himaya ya umangi Old Moshi.

– Hivyo ukoo wa Kiwia unapatikana kwa kiasi kwenye baadhi ya vijiji vya Uru, Mashariki.

– Ukoo wa Kiwia unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Tela, Old Moshi.

– Ukoo wa Kiwia unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Kiwia unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Kiwia unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kmare, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kiwia unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

Ukoo wa Kiwia ina idadi kubwa sana ya wasomi lakini bado kuna uhaba wa taarifa za kuhusu ukoo husika, hivyo tunahitaji taarifa zaidi kuhusu ukoo huu ili kuimarisha tafiti na faida pia ya kizazi cha sasa na baadaye.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Kiwia.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kiwia?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kiwia?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kiwia?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kiwia una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kiwia wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kiwia kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kiwia?

9. Wanawake wa ukoo wa Kiwia huitwaje?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kiwia?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kiwia?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kiwia?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kiwia kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *