UKOO WA MBOWE.

– Ukoo wa Mbowe ni tawi la ukoo maarufu uliogawanyika na matawi yake kusambaa Uchaggani kote wakitumia majina tofauti tofauti uliojulikana kama Mboro. Tawi hili la ukoo wa Mbowe lina asili yake katika eneo la vijiji vilivyopo upande wa mashariki na magharibi ya kingo za mto Weruweru, ambapo unapatikana kwa wingi zaidi katika kijiji cha Nshara, Machame kilichopo upande wa magharibi wa mto Weruweru na vijiji vya kata ya Narumu, Machame vilivyopo upande wa mashariki wa mto Weruweru.

– Ukoo huu wa Mbowe ambao unapatikana kwa wingi pia katika eneo la Narumu mashariki wa mto Weruweru umekuwa ni sehemu ya jamii ya watu mahodari wa ufinyanzi sambamba na koo nyingine asili za eneo hili kama vile Kweka. Hivyo vizazi vingi vilivyopita vya wachagga wa ukoo wa Mbowe wamekuwa sehemu ya ujuzi huu uliopata umaarufu Kilimanjaro nzima na kuwa na wateja wengi maeneo mengi mashariki na magharibi ya Uchagga, Kilimanjaro.

– Wachagga wa ukoo wa Mbowe ni watu wenye asili ya kujituma sana na baadhi wamefanikiwa kufanya mambo makubwa katika maeneo mbalimbali kwenye maisha ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania. Ni ukoo uliotoa wafanyabiashara, wanaharakati, wasomi na na watu wenye ari kubwa ya kufanikisha makubwa katika maisha na baadhi wameweza kufikia viwango vya juu katika hayo.

– Ukoo wa Mbowe kama tawi kutoka kwenye ukoo mama wameweza kuongezeka idadi na kusambaa kwenye vijiji vingine vya Uchagga na hata kuongezeka pia idadi sana kwenye vijiji vyao, hivyo ukoo wa Mbowe wanapatikana kwa uchache sana kwenye baadhi ya vijiji vya Masama.

– Ukoo wa Mbowe wanapatikana kwa kiasi kidogo katika kijiji cha Uduru, Machame.

– Ukoo wa Mbowe wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Nshara, Machame.

– Ukoo wa Mbowe wanapatikana kwa wingi sana pia katika vijiji vya kata ya Narumu, Machame.

Hata hivyo ukiachana na taarifa kuhusu ukoo wa mama tunahitaji kupata taarifa zaidi kuhusu ukoo huu mashuhuri wa Mbowe kwa ajili ya kuongeza kwenye tafiti na kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye kuweza kujenga kujitambua na kujiamini zaidi (self esteem).

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Mbowe.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mbowe?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mbowe?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mbowe?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mbowe una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Mbowe wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mbowe kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mbowe?

9. Wanawake wa ukoo wa Mbowe huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mbowe?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mbowe?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mbowe?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mbowe kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *