– Mboya ni ukoo mkubwa na maarufu wa kichagga uliosambaa katika vijiji mbalimbali vya Uchagga, Kilimanjaro na katika maeneo mengi mbalimbali pia. Kiuhalisia ukoo wa Mboya ni tawi la ukoo wa Mboro. Ukoo wa Mboro ambao ulikuwa ni ukoo mkubwa sana na mashuhuri sana uliosambaa kila mahali Uchaggani, Kilimanjaro na uliokuwa unaheshimika sana zamani ulikuja kugawanyika katika matawi mengi yaliyosambaa sana ambapo tawi mojawapo mashuhuri sana ni hili la ukoo wa Mboya.
– Kutoka kwenye historia tawi la ukoo wa Mboya kutokea kwenye ukoo wa mama wa Mboro liliweza kusambaa na kupatikana maeneo mengi zaidi ya Uchaggani kuanzia magharibi mpaka mashariki. Ukoo wa Mboya ni ukoo wa watu wenye kujituma sana na wanaofanya vizuri maeneo ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.
– Hivyo ukoo wa Mboya unapatikana kuanzia magharibi katika kitongoji cha Nkweseko, kijiji cha Foo, Machame.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Orori, kata ya Narumu, Machame.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Manushi chini, Kibosho.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Umbwe, Kibosho.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kindi, Kibosho.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Sambarai, Kibosho.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Omarini, Kibosho.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mloe, Kibosho.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kitandu, Kibosho.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Tema, Mbokomu, Old Moshi.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kyou, Kilema.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ruwa, Kilema.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Makami Juu, Kilema.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Makami Chini, Kilema.
– Ukoo wa Mboya unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mboni, Mamba.
Tunahitaji kupata taarifa zaidi juu ya ukoo huu wa Mboya na namna matawi yalivyoachana kutoka kwenye ukoo mama wa Mboro. Tunahitaji kufahamu zaidi kuhusu watu wa ukoo huu ili kuweza kufahamiana zaidi na kujenga mshikamano imara kuelekea kufanya mambo makubwa katika ngazi mbalimbali na tasnia mbalimbali. Taarifa zitakazosaidia kujenga hamasa zaidi na kuimarisha umoja wa wanaukoo na wachagga kwa ujumla.
Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Mboya.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mboya?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mboya?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mboya?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mboya una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Mboya wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mboya kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mboya?
9. Wanawake wa ukoo wa Mboya huitwaje, na kwa nini?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mboya?
11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mboya?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mboya?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mboya kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).
Whatsapp/Call +255 754 584 270.