UKOO WA NYELLA.

– Nyella ni ukoo wa wachagga wanaopatikana zaidi katika eneo la katika la ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro na kiasi katika eneo la mwanzoni la ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu wengi wasomi na wanaofanya vizuri sana kwenye taasisi mbalimbali za ndani na za kimataifa na hata kwenye biashara na ujasiriamali pia.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Nyella hauonekani kuzungumziwa sana na hata kwenye kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga”ambacho kimezungumzia eneo la wafua vyuma wa himaya ya umangi Mamba ikiwa ni moja ya sehemu wanakopatikana ukoo wa Nyella unaojishughulisha na hili lakini haujazungumziwa sana wenyewe kipekee. Hata hivyo unatambulika sana eneo hili na baadhi kwenye shughuli hizi za uhunzi.

– Ukoo wa Nyella umesambaa zaidi na unapatikana japo sio kwa wingi sana lakini katika vijiji vya maeneo ya ukanda wa mashariki ya kati na ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro.

– Ukoo wa Nyella unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Komakundi, Mamba.

– Ukoo wa Nyella unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Maring’a, Mwika.

– Ukoo wa Nyella unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Nyella unapatikana kwa wingi kiasi sehemu za Mahida, Rombo.

Ukoo wa Nyella ni ukoo wenye wasomi wengi na watu wenye weledi mkubwa. Hata hivyo bado hakuna maudhui mengi yaliyoandikwa kuhusu ukoo huu, hivyo kuna maswali mengi ambayo hayajajibiki kuhusu ukoo wa Nyella. Tunahitaji kufahamu mengi zaidi kuhusu ukoo wa Nyella ili kuhifadhi maudhui mengi zaidi katika maktaba ya ukoo huu na jamii ya wachagga kwa ujumla. Tunahitaji kuhifadhi taarifa na maudhui katika maktaba za mitandaoni na maktaba halisi pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja kujitambua na kujijengea kujiamini zaidi kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Nyella.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Nyella?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Nyella?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Nyella?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Nyella una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Nyella wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Nyella kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Nyella?

9. Wanawake wa ukoo wa Nyella huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Nyella?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Nyella?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Nyella?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Nyella kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *