– Makoi ni ukoo wa wachagga unaopatikana zaidi katika ukanda wa magharibi ya karibu ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Makoi ni watu wenye sifa ya kuwa majasiri sana huku wengi wakiwa ni watu wanaofanya vizuri sana kwenye maisha hasa katika biashara na ujasiriamali.
– Ukoo wa Makoi pia ni ukoo unaotoa watu wengi wanaokuwa mbele katika uongozi na hata siasa kwa ujumla, kwa ni watu wanaojiamini sana hujikuta wakifika katika ngazi za juu za uongozi katika nyanja zote za kwenye maisha wanapokuwepo.
– Ukoo wa Makoi ambao chimbuko lake kwa Uchaggani, Kilimanjaro huenda ni katika kijiji cha Mkomilo, Kibosho umesambaa na unapatikana katika vijiji zaidi katika eneo hili la magharibi ya karibu ya Uchagga, Kilimanjaro.
– Hivyo, ukoo wa Makoi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Umbwe, Kibosho.
– Ukoo wa Makoi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mloe, Kibosho.
– Ukoo wa Makoi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mkomilo, Kibosho.
– Ukoo wa Makoi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kindi Muyuni, Kibosho.
Ukoo wa Makoi japo sio ukoo mkubwa lakini ni ukoo wa watu wenye uthubutu wa kipekee. Huu ni ukoo ambao licha ya kuwa na wasomi wengi pia lakini bado hakuna maudhui mengi yaliyoandikwa kuhusu ukoo huu, hivyo kuna maswali mengi ambayo hayajajibiki kuhusu ukoo wa Makoi. Tunahitaji kufahamu mengi zaidi kuhusu ukoo wa Makoi ili kuhifadhi maudhui mengi zaidi katika maktaba ya ukoo huu na jamii ya wachagga kwa ujumla. Tunahitaji kuhifadhi taarifa na maudhui katika maktaba za mitandaoni na maktaba halisi pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja kujitambua na kujijengea kujiamini zaidi kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha katika ngazi ya mtu mmoja mmoja kwenye ukoo, ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.
Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Makoi.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Makoi?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Makoi?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Makoi?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Makoi una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Makoi wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Makoi kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Makoi?
9. Wanawake wa ukoo wa Makoi huitwaje, na kwa nini?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Makoi?
11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Makoi?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Makoi?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Makoi kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).
urithiwetuwachagga@gmail.com
Whatsapp +255 754 584 270.