– Ringo au zamani ulikuwa ukiitwa pia Iringo ni ukoo mkongwe sana wa kichagga unaopatikana katika maeneo kadhaa ya vijiji vya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Ringo wengi ni wapambanaji sana wakiwa wamesambaa maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania wakifanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali. Mmoja kati ya …
Category: Makala
UKOO WA NGOWI.
– Ngowi ni ukoo mkubwa maarufu na mashuhuri sana wa wachagga uliosambaa katika vijiji vingi sana na katika maeneo mengi sana ya Uchagga, Kilimanjaro. Kuna wachagga wengi sana wa ukoo wa Ngowi ambao wanafanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali ya kimaisha ndani na nje ya Kilimanjaro, nje ya Tanzania na Afrika mashariki. – Kutoka kwenye …
UKOO WA CHUWA.
– Chuwa ni ukoo maarufu wa wachagga ambao na wenye idadi kubwa kiasi ya watu ukiwa na watu mbalimbali waliosambaa maeneo mengi ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania. Wachagga wa ukoo wa Chuwa wengi ni watu wenye kujituma sana na wakiwa na wafanyabiashara wengi wanaofanya vizuri ndani na nje ya Kilimanjaro …
UKOO WA TILLYA.
– Tillya ni ukoo mkongwe sana wa kichagga na ulioenea katika vijiji vingi mbalimbali ndani ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu wengi wanaopatikana katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi. Wachagga wa ukoo wa Tillya ni watu wenye kujituma na wanafanya vizuri sana katika taaluma zao na …
MACHAME, MASAMA – MARIRE
Urithi Wetu Wachagga. urithiwetuwachagga@gmail.com Whatsapp +255 754 584 270.
UKOO WA MUSHI/MOSHI.
– Mushi/Moshi ni ukoo mmoja mkubwa sana unaopatikana katika vijiji vingi zaidi Uchaggani, Kilimanjaro pengine kuliko ukoo mwingine wowote wa kichagga ikiwemo ukoo wa Massawe. Kwa mujibu wa takwimu za google kuhusu idadi ya majina ya ukoo, Mushi/Moshi unaonekana ndio ukoo wa kichagga wenye idadi kubwa zaidi ya watu ukipatikana kwa wingi maeneo mengi na …
UKOO WA OTTARU.
– Ottaru ni ukoo wa wachagga wenye chimbuko lao kwa Uchaggani katika kijiji kinachojulikana kama Otaruni, Kibosho. Hata hivyo ukoo huu wa Ottaru unaonekana ukipatikana kwa wingi zaidi katika kijiji cha Kirima kuliko kwenye chimbuko lao huko Otaruni ambako kuna mchanganyiko wa koo hususan ukoo wa Massawe. – Kutoka kwenye simulizi za wazee wenyewe wa …
UKOO WA MBOWE.
– Ukoo wa Mbowe ni tawi la ukoo maarufu uliogawanyika na matawi yake kusambaa Uchaggani kote wakitumia majina tofauti tofauti uliojulikana kama Mboro. Tawi hili la ukoo wa Mbowe lina asili yake katika eneo la vijiji vilivyopo upande wa mashariki na magharibi ya kingo za mto Weruweru, ambapo unapatikana kwa wingi zaidi katika kijiji cha …
UKOO WA TARIMO.
– Tarimo ni ukoo mkubwa sana, maarufu sana na mashuhuri sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro. Huu ni ukoo ambao umekuwa ukoo mama kwa baadhi ya koo na ni moja kati ya koo zinapatikana karibu kila mahali Uchaggani. Ukoo wa Tarimo ni mkongwe sana na unafahamika kusambaza vizazi vyake katika maeneo mengi ya Uchagga tangu …
UKOO WA KIWIA.
– Kiwia ni ukoo wa wachagga uliosambaa katika vijiji kadhaa ndani ya Uchagga hususan maeneo ya katikati ya Uchagga. Japo sio ukoo mkubwa sana lakini wachagga wa ukoo wa Kiwia ni watu wenye kujituma sana na wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania. – Kutoka kwenye historia …