“THE JEWISH PHENOMENON” “SEHEMU YA 7” Siri 7 Zilizowasaidia Wayahudi Kuwa na Utajiri Mkubwa na wa Kudumu

“THE JEWISH PHENOMENON”

“SEHEMU YA 7”

Siri 7 Zilizowasaidia Wayahudi Kuwa na Utajiri Mkubwa na wa Kudumu.

WATU WENYE MAFANIKIO MAKUBWA KIUCHUMI NI WANATAALUMA NA WAJASIRIAMALI.

Wayahudi wanatambua vizuri sana kwamba mafanikio makubwa kiuchumi hupatikana kupitia taaluma na ujasiriamali au biashara.

-Udaktari, uanasheria na biashara ni vitu ambavyo wayahudi wamekuwa wakivizungumzia zaidi pale wanapozungumzia kazi za kufanya.

-Kuwa kuwa mtaalamu wa taaluma Fulani(professional) kama vile daktarin bingwa au wakili mashuhuri au kuwa mjasiriamali au kumiliki biashara yako mwenyewe ni kazi ambazo huwa zina kipato kikubwa kuliko wastani wa mishahara ya kawaida ni mwanzo mzuri wa kuelekea kutengeneza utajiri. Wayahudi wengi huchagua moja kati ya kuwa mtaalamu wa taaluma fulani au kuwa mjasiriamali. Hata wazazi wao huanza kuwajengea mitazamo hiyo mapema sana na kuwahimiza kuchagua kazi hizi ambazo mwisho wa siku huwa na kipato kizuri.

-Mpaka kufikia miaka ya 1950’s asilimia 20% ya wayahudi walikuwa ni wataalamu wa taaluma fulani huku asilimia 35% wakiwa ni wamiliki wa biashara na wajasiriamali hiyo ikiwa ni mara tatu zaidi kwa wastani ukilinganisha na jamii nyingine. Kufikia miaka ya 1950’s zaidi ya 55% ya wayahudi walikuwa wanafanya kazi za maofisini yenye kipato kikubwa na cha uhakika ukilinganisha na jamii nyingine ambazo wengi bado walikuwa kwenye vibarua na kipato kidogo kisichokuwa cha uhakika.

-Kufikia miaka ya 1970’s wataalamu wa mambo ya kijamii wamewataja wayahudi kama jamii ya kwanza duniani ambayo watu wake wote wanafanya kazi za maofisini au kwenye nafasi za usimamizi huku wakiwa hawana kabisa watu katika jamii yao wanaofanya kazi kama vibarua au kazi za mikono.

-Wayahudi wamekuwa ni watu wanaoongoza kwa kujiongeza sana kielimu kwani katika chuo cha Harvard peke yake cha nchini Marekani ambacho kinapokea wanafunzi bora kabisa kutoka dunia nzima asilimia 15% ya wanafunzi wanadahiliwa Harvard University kujiunga na shahada ya uzamili na shahada ya uzamivu baada ya digrii ya kwanza ni wayahudi.

-Baada ya shahada ya pili au tatu wayahudi wamekuwa wakiingia katika ubobevu wa kitaaluma kwa kasi zaidi sasa kuliko wakati mwingine wowote katika historia na kisha kuanzisha kampuni mbalimbaki zinazotoa ushauri wa kitaaluma kama vile sheria, udaktari, uhandisi, uhasibu n.k., taaluma ambazo zinawapa kipato kizuri na mwanzo mzuri wa kukusanya utajiri.

-Wayahudi wamekuwa ni madaktari wazuri wa tiba asilia kwa karne nyingi katika historia kwani nyakati za “medieval” huko Ulaya asilimia 50% ya madaktari walikuwa ni wayahudi na hivyo kuwa na mchango mkubwa sana huko Ulaya, hivyo imekuwa ni sehemu ya utamaduni wao kufanya vizuri katika taaluma ya afya.

-Ari ya ujasiriamali imekuwa na nguvu sana ndani ya jamii ya wayahudi na imewasaidia kupiga hatua sana kiuchumi na kukusanya utajiri mkubwa.

-Wastani wa wayahudi waliojiajiri ndani ya Marekani ni mara mbili zaidi ya jamii nyingine licha ya kwamba kwa miaka mingi nyakati za nyuma wamekuwa wakipigwa marufuku au kuwekewa vizuizi katika kujihusisha na baadhi ya biashara nchini humo. Pia wamekuwa wakiwekewa vizuizi katika kupata kazi kadhaa hivyo wengine wamelazimika kujiajiri zaidi.

-Wayahudi wamewekeza katika biashara ya ardhi na majengo(real estate) ambapo katika orodha ya mabilionea wakubwa katika uwanja huo wa real estate zaidi ya asilimia 35% ya mabilionea hao ni wayahudi. Wayahudi wengi waliingia Marekani wakiwa maskini kutokea nchi za Ulaya na kuanza kama madalali wa majengo na kisha kutumia vizuri kamisheni hizo kuwekeza mpaka sasa wamekuwa wamiliki wakubwa wa majengo Marekani hasa katika jiji la New York, wamewekeza sana pia katika mahoteli makubwa.

-Wayahudi wamekuwa na mafanikio sana katika sekta ya fedha na mabenki kwa sababu kwanza dini yao haikatazi kutoza riba katika fedha na mikopo. Hii ni tofauti na sheria za kanisa katoliki ambazo zilipitishwa miaka ya zamani ya “medieval” kwamba kutoza riba ni dhambi na kupiga marufuku riba hivyo kupelekea mabenki mengi kufilisika, wayahudi waliweza kutumia fursa hiyo kufanikiwa sana kiuchumi kwani dini yao haikuwa inahesabu kama rib ani dhambi.

-Wayahudi baada ya kuwekewa vikwazo sana kwenye umiliki wa benki za biashara(commercial banking) walikuwa watu wa mwanzo walionzisha wazo la benki za uwekezaji(investment banking) zenye maslahi zaidi kuliko benki za biashara na zilizowapa mafanikio makubwa.

-Wayahudi wamewekeza sana pia kwenye masoko ya hisa na mitaji maarufu kama “Wall Street” nchini Marekani ambayo ni moja ya vitovu vya wawekezaji wa wakubwa na kwenye utajiri mkubwa sana nchini Marekani.

-Wayahudi wamewekeza sana pia katika maduka makubwa ya jumla na reja reja yenye matawi mbalimbali kote nchini Marekani.

-Wayahudi wamewekeza pia kwenye madini kwa wingi sana na wana umiliki mkubwa katika makampuni makubwa ya madini Afrika, sambamba na masonara ya kutengeneza vito vya thamani maarufu kama Jewelry. Hata kampuni ya DeBeers ya Afrika kusini nusu yake ilikuwa inamilikiwa na wayahudi.

-Wayahudi wamekeza sana pia katika makampuni ya teknolojia kama kompyuta na kampuni za teknolojia za mitandao kama facebook, whatsapp, google n.k.,.

Ari na hamasa ya ujasiriamali inayopandikizwa tangu utotoni ambayo mara nyingi siku zote ndio msingi wa utajiri mkubwa imewasaidia wayahudi kupiga hatua kubwa sana kimaendeleo.

MAMBO AMBAYO SISI KAMA WACHAGGA TUNAWEZA KUJIFUNZA NINI KUTOKA KWA WAYAHUDI

-Tuweke bidii kwenye taaluma zetu lakini ni vyema tukajiandaa pia kuingia kwenye ujasiriamali.

Ni vizuri tunapoanza na taaluma fulani ili kujenga uwezo, mtaji pamoja na kujenga mtandao wa marafiki na watu wenye manufaa wanaoweza kusaidia kupata maarifa zaidi, mtaji, koneksheni na mawazo bora zaidi kuelekea kule unakolenga kufika.

-Licha ya kwamba tunaweza kuwa na taaluma tunazozifanya lakini tutenge muda wa kujifunza na kufanya ujasiriamali.

Usifanye ajira moja kwa moja ukajisahau badala yake uweke malengo makubwa ya pembeni ya kujiajiri na kufanya vizuri katika ajira yako binafsi wakati bado unaendelea na ajira uliyopo kwa sasa.

-Kujaribu kuwekeza kwenye fursa ambazo zinaonekana kuwa na manufaa lakini hazizungumziwi sana wala sio maarufu kutoka kwenye taaluma yako.

Unaweza kuangalia eneo fulani ndani ya taaluma yako ambalo watu wengi hawalioni au wanalipuuza na ukalipa nafasi, ukajifunza ukiendelea kufikiria namna utalipatia suluhisho kwa watu kisha kulitumia kupiga hatua kimaendeleo. Hivi ndivyo wajasiriamali wengi wametajirika na kupata mafaniko makubwa kwa kuweka nguvu kwenye eneo dogo, kisha kuja na suluhisho lililowasaidia watu wengi.

Ahsanteni

Tutaendelea na siri ya nne kwenye makala inayofuata.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

  1. Mimi siyo mchagga lakini nimeolea uchaggani, Mkuu – Rombo. Napendezwa na makala nzuri za kurasa huu kwakuwa Kuna mengi ya kujifunza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *