UKOO WA MARIKI.

– Ukoo wa Mariki ni ukoo mkongwe sana wa kichagga na maarufu zaidi upande wa mashariki na kati ya Kilimanjaro. Huu ni ukoo uliotoa watu kadhaa mashuhuri ambao wamekuwa na umuhimu mkubwa katika historia ya wachagga Kilimanjaro kama vile Mzee Makiponyi Mariki aliyekuwa baba mlezi wa Mangi Ndegoruo Marealle baada ya kumuoa mama yake aliyeitwa Nderero.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Mariki umekuwa ni ukoo wenye nguvu na uliotawala eneo la Msae, Mwika ambalo mwanzoni lilikuwa ni himaya ndogo ya Msae kwa karne nyingi katika historia. Inasemekana kwamba mwanzoni ukoo wa Mariki walikuwa wakiishi katika ukanda wa juu wa sana wa eneo la Msae ambalo kwa sasa ni eneo la msitu wa mlima Kilimanjaro kabla ya baaaye kushuka na kuweka makazi ya kudumu katika vijiji ambavyo ndio Msae kwa sasa.

– Historia inaeleza kwamba wakati ukoo wa Mariki wanateremka na kuweka makazi yao ya kudumu katika eneo la Msae, Mwika walikuta tayari ukoo wa Mlay walishatangulia wakiishi katika eneo hilo hilo la Msae. Hata hivyo ukoo wa Mariki ndio waliotawala eneo hilo lililokuja kuwa himaya ndogo ya umangi isipokuwa wakati wa utawala wa Mangi Horombo mwanzoni mwa karne ya 18 ambapo Horombo alimteua Tenguti kutoka ukoo wa Mlay kutawala Msae kama kibaraka wake. Baada ya utawala wa Mangi Horombo kuanguka ukoo wa Mlay uliendelea kutawala Msae mpaka utawala wa Tenguti ulipoanguka na Msae kuendelea kutawaliwa na ukoo wa Mariki.

– Mtawala wa mwanzoni na mkongwe zaidi wa ukoo wa Mariki anayekumbukwa na historia aliitwa Mrimiya na kwa kuhesabu vizazi anaonekana aliishi mwanzoni au katikati ya karne ya 18. Mtawala mwingine wa ukoo wa Mariki aliyekuja kupata umaarufu sana katika historia aliitwa Lengaki na alikuwa mtawala wa eneo hili la Msae mwishoni mwa karne ya 19 wakati wa utawala wa Mangi Ndegoruo Marealle wa Marangu.

– Mtawala wa mwisho kutokea kwenye ukoo wa Mariki aliitwa Mchili na alitawala eneo la Msae mpaka mwanzoni mwa karne ya 20 kabla ya kuondolewa madarakani na Msae kuweka chini ya utawala wa himaya ya umangi Mwika. Mivutano ya kisiasa ndani ya ukoo wa Mariki iliendelea mpaka kwenye Chagga Council wakati wakiwakilisha kama wachili kutoka Msae.

– Ukoo wa Mariki kutokea Msae, Mwika umeendelea kusambaa sehemu kubwa zaidi ya Uchagga, Kilimanjaro na idadi ya watu kuongezeka sana.

– Hivyo wachagga wa ukoo wa Mariki wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Arisi, Marangu.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mshiri, Marangu.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mmbahe, Marangu.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkolowony, Mamba.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kidogo katika kijiji cha Komakundi, Mamba.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lekura, Mamba.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Msae Kinyamvuo, Mwika.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Lole Marera, Mwika.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Lole, Mwika.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kondiki, Mwika.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mwika, Mwika.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana katika kijiji cha Maring’a Mwika.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Shokony, Mwika.

– Ukoo wa Mariki wanapatikana katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

Ukoo wa Mariki umekuwa ni ukoo wenye historia ndefu na ikiwa ni sehemu muhimu sana ya historia ya wachagga Kilimanjaro sambamba na kutoa watu mbalimbali mashuhuri lakini taarifa zake nyingi zimepotea. Hivyo tunahitaji mchango wa mawazo zaidi juu ya taarifa za ukoo huu muhimu ili kuweza kuchangia kwenye tafiti sambamba na kuongeza maudhui zaidi ya ukoo husika. Taarifa hizo zitasaidia kuhamasisha mshikamano zaidi kuelekea kufanikisha mambo makubwa kwa ukoo husika kwa ngazi ya ukoo na hata ngazi ya mtu mmoja mmoja ndani ya ukoo.

Karibu kwa mchango zaidi wa mawazo.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mariki?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mariki?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mariki?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mariki una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Mariki wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mariki kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mariki?

7. Wanawake wa ukoo wa Mariki huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mariki?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mariki?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *