– Ukoo wa Mallya ni ukoo mkubwa mashuhuri na maarufu sana Uchaggani kwa ujumla. Huu ni ukoo unaohusishwa na watu wengi wenye ujasiri mkubwa katika kukabiliana na mambo mbalimbali katika maisha kwa ujumla.
– Kutoka kwenye historia ukoo wa Mallya kwa Uchaggani, Kilimanjaro unaonekana kuwa na chimbuko lake katika vijiji vya ukanda wa juu Kibosho hususan katika kijiji cha Sisamaro. Ukoo wa Mallya wa maeneo hayo hususan katika eneo la Kibosho Maro katika kijiji cha Sisamaro walikuwa ni wachagga wenye nguvu kubwa ya ushawishi wa kisiasa na walioweza hata kuwa tishio kwa watawala.
– Ukoo huu wa Mallya kutokana na kuwa na watu wengi jasiri na wenye kujiamini sana wameweza kuwa na watu wanaofanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi. Ukoo wa Mallya licha ya kuwa na matawi pia ndani ya Uchagga lakini wameweza kuongezeka sana idadi na kusambaa maeneo mengine mengi ndani ya Uchaggani hususan ndani ya Kibosho.
– Hivyo ukoo wa Mallya unapatikana kwa kiasi katika baadhi ya vijiji vya himaya ya umangi Siha/Sanya Juu.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nkuu, Machame.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa kiasi katika vijiji vya kata ya Lyamungo, Machame.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Umbwe Ndoo, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kifuni, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Umbwe Kati, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Umbwe Onana, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa wingi katika vijiji vya Manushi Ndoo na Manushi Sinde, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana katika vijiji vya kata ya Kindi, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana katika kijiji cha Sambarai, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana katika kijiji cha Otaruni, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana katika kijiji cha Maua, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa wingi sana katika Mkomongo, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kombo, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Omarini, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Sisamaro, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Dakau, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana katika kijiji cha Mkomilo, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana katika kijiji cha Uri, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana katika kijiji cha Kitandu, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana katika kijiji cha Mloe, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana katika kijiji cha Kirima Juu, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana katika kijiji cha Kirima Kati na Boro, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana katika kijiji cha Singa Juu na Singa chini, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana katika kijiji cha Sungu, Kibosho.
– Ukoo wa Mallya unapatikana katika baadhi ya vijiji vya Uru.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nduoni, Kirua Vunjo.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lekura, Mamba.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa kidogo katika kijiji cha Kondeni, Mwika.
– Ukoo wa Mallya unapatikana kwa kiasi kidogo sana kwenye baadhi ya vijiji vya Rombo.
Lakini pamoja na ukubwa wa ukoo wa Mallya na umashuhuri wake bado kuna taarifa chache sana tulizonazo kuhusiana na ukoo huu wenye sifa za kipekee. Tunahitaji mchango zaidi wa mawazo juu ya ukoo wa Mallya ili kuweza kuongeza katika utafiti sambamba na kuongeza maudhui zaidi ya ukoo husika ili kuhamasisha mshakamano zaidi miongoni mwa wanaukoo kuelekea kufanya mambo makubwa zaidi kwa ngazi ya ukoo na kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja wa ukoo wa Mallya.
Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mallya?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mallya?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mallya?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mallya una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Mallya wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mallya kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mallya?
9. Wanawake wa ukoo wa Mallya huitwaje?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mallya?
11. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mallya?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na ukoo wa Mallya?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mallya kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.
Whatsapp +255 754 584 270.