UKOO WA MASSAM.

– Massam ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi sana maeneo ya katikati au mashariki ya karibu ya Uchagga na maeneo ya mwishoni mwa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Massam ni ukoo wa watu jasiri sana na wanaofanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya …

UKOO WA SOMI.

– Somi ni ukoo wa wachagga ukiwa moja kati ya koo zinazopatikana kwa uchache sana Uchaggani, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Somi wanapatikana kwa kiasi kwenye baadhi ya vijiji katika maeneo ya magharibi ya kati ya Uchagga hususan katika eneo la Machame central lakini ukipatikana pia kwa uchache katika maeneo ya katikati ya Uchagga, Kilimanjaro. …

UKOO WA SILAYO.

– Silayo ni ukoo mkubwa kichagga na maarufu sana wa wachagga unaopatikana kwa wingi sana upande wa kuanzia mwishoni mwa mashariki ya kati mpaka mashariki ya mbali kabisa ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Silayo wamesambaa sana ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi wakiwa wanafanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali …

UKOO WA URONU.

– Uronu ni ukoo wa wachagga wanaopatikana maeneo ya magharibi ya kati ya Uchaga, Kilimanjaro. Ukoo huu nao kuna tetesi kwamba ni sehemu ya zile koo zilizotokana na ukoo mkubwa kabisa Kilimanjaro uliogawanyika na kutengeneza koo nyingi sana, ukoo wa Mboro. – Wachagga wa ukoo wa Uronu wanapatikana zaidi katika vijiji vichache lakini ni watu …

UKOO WA SARIA.

– Saria ni ukoo wa wachagga unaopatikana kwa wingi maeneo ya mashariki ya karibu au katika ya Uchagga, Kilimanjaro na maeneo ya mwishoni mwa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Saria japo sio ukoo wenye idadi kubwa sana ya watu lakini ni ukoo wenye mchanganyiko wa baadhi ya watu makini wanaofanya vizuri katika …

UKOO WA MALEKO.

– Maleko ni ukoo maarufu wa wachagga wanaopatikana zaidi maeneo ya mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Maleko wengi ni watu makini na wasomi sana na wanaofanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali katika maisha hasa taaluma na biashara katika taasisi za umma, taasisi binafsi na kwenye taasisi za kimataifa. – Kutoka kwenye historia …

UKOO WA OLOMI/ULOMI.

– Olomi/Ulomi ni ukoo mkubwa kiasi wa wachagga wanaopatikana kwa wingi upande wa magharibi na magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro na kwa kiasi katikati ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu wengi waliosambaa maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi. – Chimbuko halisi la ukoo wa Olomi/Ulomi …

UKOO WA CHAMI

– Chami ni ukoo mkubwa wa wachagga wanaopatikana upande wa magharibi ya kati kuelekea magharibi zaidi ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Chami ni kati ya koo ambazo kihistoria ziliweza kutoa watu hodari na mashuhuri katika utaalamu wa ufinyanzi na wafanyabiashara wa bidhaa za ufinyanzi hususan vyombo vya nyumbani. – Vyombo vingi vya nyumbani vilivyotengenezwa na …

UKOO WA SHAO.

– Shao ni mkubwa wa wachagga wanaopatikana katika ukanda wa mwishoni mwa mashariki ya kati na mashariki zaidi ya Uchagga, Kilimanjaro. Baadhi ya watu huwa hawawezi kuutofautisha ukoo wa “Shao” na ukoo mwingine maarufu wa “Shayo”. Hata hivyo baadhi ya watu wa ukoo wa Shao wanaamini kwamba wao ni ukoo mmoja na Shayo na wengine …

UKOO WA MUNISHI.

– Munishi ni ukoo maarufu wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi maeneo ya magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Munishi ni ukoo mkubwa wenye watu wengi lakini pia wenye utata fulani nyuma yake kutokana na kuhusianishwa na koo nyingine za kichagga zinazoshabihiana nao kwa majina. – Kuna dhana inayoaminika kwamba kuna uhusiana wa …