TEKNOLOJIA YA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI KATIKA NCHI YA WACHAGGA.


– Jamii Yoyote Ili Iweze Kupiga Hatua Kubwa Kimaendeleo Katika Nyanja Zake Zote Inapaswa Kuwekeza Sana Kwenye Maendeleo Ya Kiteknolojia. Na Jamii Yoyote Inayoweka Juhudi Kubwa Kwenye Kuhimiza Kuchochea na Kukuza Teknolojia Zake Katika Nyanja Mbalimbali Huweza Kukua Haraka Kwani Inarahisisha Sana Mifumo Yake Ya Kiuchumi Katika Utengenezaji wa Thamani Ambao Kimsingi Ndio Utajiri wa Jamii Husika.


– Duniani Kote Tumeweza Kuona Jinsi Zile Nchi Zilizowekeza Kwenye Kukuza Teknolojia Katika Nyanja Mbalimbali na Kuziunganisha Teknolojia Hizo Ndani Ya Mifumo Mbalimbali Inayounganishwa Pamoja Zilivyo Mbali Kimaendeleo. Lakini Teknolojia Hizi Hazikuanzia Juu Hapo Zilipo Bali Zilianza Taratibu na Baada Ya Muda Mrefu Zinakuwa Zimefika Mbali Sana. Hata Hivyo Mkwa Miaka Ya Sasa Ambapo Dunia Ina Mwingiliano Mkubwa Unaweza Kuiga Maarifa Ya Teknolojia Hizo Kutoka Maeneo Mengine Duniani na Kuziendeleza Kuzitumia Katika Nchi Nyingine.


– Hata Hivyo Wote Tunafahamu Kwamba Maendeleo Ya Teknolojia Yanahusisha Kuweka Juhudi Kubwa Sana Ya Akili Katika Kufanikiwa Kufikia Viwango vya Juu Vya Teknolojia Hizo. Maendeleo Makubwa Ya Teknolojia Yanayoonekana Duniani Leo Ni Matokeo Ya Watu Kuwekeza Nguvu Kubwa Sana Ya Akili na Fikra Katika Kuendeleza Ubunifu Ulioweza Kufikia Hapo. Baadhi Ya Watu Wasiojua Kanuni za Asili za Maisha Huweza Kufikiri Kwamba Kuna Ushirika au Miujiza Inayopelekea Watu Kufikia Viwango vya Juu Vya Teknolojia Mbalimbali Kama Zinavyoonekana Sasa Duniani. Lakini Ukweli Ni Kwamba Hayo ni Matokeo Ya Bidii Kubwa Ya Kuwezekeza Akili na Fikra Katika Eneo Husika Kwa Muda Mrefu na Kwa Kujitoa Sana.


– Tukirudi Nyumbani Katika Nchi Ya Wachagga Moja Kati Ya Eneo La Kiteknolojia Ambalo Wachagga Waliweka Akili na Ubunifu Mkubwa Ambao Uliwashangaza Hata Wageni Wengi Waliotembelea Kilimanjaro ni Katika Eneo La Umwagiliaji wa Mashamba Kwa Kutumia Mirefeji(Mifongo) Ya Maji. Wachagga Katika Kukabiliana na Janga La Njaa na Kudumaa Kwa Mifugo Kutokana na Kutegemea Maji Ya Mvua Peke Yake Waliwekeza Uwezo Mkubwa wa Kiakili Katika Kuja na Teknolojia Kubwa Sana Ya Mifereji Iliyowahakikishia Upatikanaji wa Maji Ya Kutosha Kwa Shughuli za Umwagiliaji na Kunywesha Mifugo.


– Akizungumzia Teknolojia Hii Kubwa Ya Umwagiliaji Aliyoikuta Kilimanjaro Alipofika Katika Karne Ya 19 na Kumshangaza Sana, Mmisionari wa Kifaransa Alexander Le Roy Alisema Hivi, “Kimsingi Wachagga na ni Lazima Ikubalike Kwamba Kati Ya Wakulima wa Kiafrika Wachagga Wako Kwenye Nafasi Ya Peke Yao. Mfumo Wao wa Umwagiliaji ni Kipekee Kabisa. Maji Ya Mfereji Hukusanywa Kutoka Upande Mwingine Kabisa wa Msitu Usiokaliwa Kabisa na Watu Kisha Kupitishwa Kwenye Miteremko na Miinuko Ya Milima na Kwenye Kingo za Miinuko na Mabonde Marefu Sana Yaliyosimama Wima, Kisha Kuteremshwa Kwenye Ukanda wa Chini Bila Hata Kuonekana Kiurahisi, Yanawekwa Kwenye Hifadhi za Mabwawa(Nduwa) Kisha Kupelekwa Katika Uelekeo Tofauti, Na Kugawanywa Katika Maelfu Ya Matawi Ya Mifereji Kupeleka Katika Kila Familia au Ukoo.” Alexander Le Roy Anaendelea Kusema, “Nitashangaa Kama Mhandisi wa Ulaya Angeweza Kufanya Kwa Ubora Zaidi Ya Huu. Hataweza Kwa Namna Yoyote Ile Nimejiridhisha na Teknolojia Yao Hii Rahisi.”


– Teknolojia Hii Ya Umwagiliaji Iliyoendelezwa na Wachagga Iliweza Kuwa na Manufaa Makubwa Kwa Wachagga Kwani Mara Nyingi Iliwaepusha na Majanga Ya Njaa Kwa Kuwahakikishia Chakula cha Kutosha na Kuilinda Mifugo Yao Dhidi Ya Kudhoofika Kiafya, Kufa au Kukosa Majani Kwani Ilihakikisha Kwamba Kwa Sehemu Kubwa Kilimanjaro Inaendelea Kuwa Ya Kijani. Hilo Liliwafanya Wachagga Kuendelea Kuwa Imara Katika Kuweka Juhudi Zaidi Katika Maeneo Mengine Ya Kukuza Uchumi Lakini Lilisababisha Pia Jamii za Nje Ya Kilimanjaro Zilizokuwa Zikikumbwa na Njaa Mara Kwa Mara Kukimbilia Kwa Wachagga, Mfano Mmojawapo ni Ile Kesi Ya Sameni Ole Kivasisi au Justin Lemenye.


– Teknolojia Hii Ya Umwagiliaji Ilikuja Kuwasaidia Tena Zaidi Wachagga Baadaye Katika Karne 20 Walipokuja Kujenga Mfumo Wa Kiuchumi Kupitia Vyama Vya Ushirika Hususan Zao La Kahawa. Teknolojia Ya Umwagiliaji Ambayo Waliiboresha Zaidi Iliwahakikishia Ustawi Bora wa Kahawa Ambayo Iliwapa Msingi Imara wa Maendeleo Ya Kisasa Katika Uchumi wa Fedha. Hili Liliwasaidia Kupata Uhakika wa Kuingiza Bidhaa Hiyo Sokoni na Hivyo Kuaminika Katika Masoko Makubwa Ya Kahawa Katika Nchi Za Ulaya.


– Hata Hivyo Baadaye Taratibu Uchumi wa Kilimanjaro Ulianza Kudorora na Hivyo Miundombinu Hii Nayo Ikaanza Kupuuzwa na Kudorora. Japo Hakuna Sababu Ya Msingi Sana Kwa nini Shughuli Hizi Zimedorora Sana Kwa Sababu Watu Wapo Siku Zote Kwani Hata Sasa Bidhaa Zote Zilikuwa Zinalimwa Miaka Ya Zamani Bado Zinahitajika Masokoni na Hata Kwa Matumizi Binafsi. Hii ni Licha Ya Kwa Msukumo Mkubwa wa Uhaba wa Ardhi.


– Je Unafikiri Kuna Haja na Namna Ya Kuboresha Tena Teknolojia Ya Umwagiliaji na Hata Kuendeleza Zaidi Kwa Sasa?


Karibu Kwa Maoni, Ushauri au Maswali.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

  1. Douglas Kavishe says:

    Kazi nzuri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *