UKOO WA TEMU.

– Temu ni ukoo mkubwa sana wa wachagga uliosambaa katika vijiji vingi sana Uchaggani, Kilimanjaro hususan kuanzia eneo la katikati kuelekea mashariki. Huu ni ukoo uliotoa watu wengi mashuhuri katika historia na watu wanaofanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi. Temu ni ukoo unaopatikana katika vijiji vingi na kwa wingi na wenye wapambanaji sana na wenye mafanikio makubwa katika kila eneo la maisha. Baadhi ya watu mashuhuri kutoka katika ukoo wa Temu ni pamoja na rafiki yangu Prof. Arnold Temu kutoka katika kijiji cha Sembeti, Marangu na mwanamitindo ambaye pia kwa sasa ni balozi Hoyce Temu kutoka katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika tawi la ukoo wa Temu wa kijiji cha Sembeti, Marangu ambao wameweza kupiga hatua kubwa kwa ngazi ya ukoo mpaka kuwa jamii ya watu wa ukoo wa Temu inayoitwa “Luwarane Society” ikimaanisha “Tushikane”, ni kwamba mzee wa zamani zaidi wa ukoo wao Temu aliitwa Masaju. Hata hivyo hakuna taarifa zaidi kama Mzee huyu Masaju anayetambuliwa na jamii ya ukoo wa Temu wa tawi la kijiji cha Sembeti, Marangu ndiye Mzee wa ukoo wote wa Temu ulioenea Uchaggani kote.

– Ukoo wa Temu pia ulitoa wachili waliokuwa kama wasaidizi wa Mangi ambao walisaidia ukoo huu kurithi mashamba makubwa na hata kuweza kutawanyika katika maeneo mengi wakishikilia mashamba makubwa na hata kutajirika. Tawi la ukoo wa Temu wa kijiji cha Sembeti, Marangu wanawataja wazee maarufu wa ukoo waliotokea kwenye kizazi cha Mzee Masaju kuwa ni Kipwe na Ngaakwi ambao alikuwa ni watoto.

– Kizazi cha Kipwe wanatajwa kwamba walikuwa ni Shikonyi, Mchomba na Malekia na kizazi cha Ngaakwi ni Matengo. Vizazi vya Shikonyi wanatajwa kuwa ni Lesiriamu, Kimangano, Ulyimali, Advesta, Chezamkonu, Ngareiya, Elinyipa, Kirikiri, Masanju na Laurent. Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu vizazi vya ukoo wa Temu kutokea kwenye jamii yao ya kiukoo ya “Luwarane Society” ambayo inalenga kuhakikisha jamii ya ukoo wa Temu inakuwa ni jamii bora yenye watu makini na yenye mafanikio makubwa sana kwa ngazi ya ukoo na kila mwanaukoo.

– Ukoo wa Temu umekuwa ni mfano wa ukoo bora ambao wameonyesha nia ya kuweka jitihada ya kuufanya kuwa ukoo bora na kuhakikisha kila mwanaukoo anakuwa na maisha yenye hadhi nzuri. Huu ni mfano unaopaswa kuigwa na koo nyingi za kichagga ambazo nyingi bado hazifanyi hivyo wala hazina utaratibu wowote wa kujaribu kuhimiza mafanikio miongoni mwa wanaukoo japo kweli zipo baadhi ambazo zinajitahidi kufanya vizuri sana.

– Kutokana na kusambaa sana kwa ukoo wa Temu ukoo huu umekuwa mkubwa sana na kuendelea kupatikana katika vijiji vingi sana Uchaggani na kwa wingi.

– Hivyo ukoo wa Temu unapatikana kwa kiasi kuanzia katika kijiji cha Umbwe, Kibosho.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa kiasi katika baadhi ya vijiji vya Uru.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kanji, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Legho, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Pofo, Kilema.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Masaera, Kilema.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kilema chini, Kilema.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ngangu, Kilema.

– Ukoo wa Temu unapatikana katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.

– Ukoo wa Temu unapatikana katika kijiji cha Makami chini, Kilema.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Makami Juu, Kilema.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Ruwa, Kilema.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Rauya, Marangu.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Sembeti, Marangu.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Kiraracha, Marangu. Karibu nusu ya kijiji cha Kiraracha ni ukoo wa Temu.

– Ukoo wa Temu wanapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Kitowo, Marangu. Karibu nusu ya kijiji cha Kitowo ni ukoo wa Temu.

– Ukoo wa Temu wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Ashira, Marangu.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kotela, Mamba.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Komakundi, Mamba.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Lekura, Mamba.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Temu unapatikana kwa kiasi katika vijiji vya kata ya Mahida, Mamsera, Rombo.

Pamoja na kwamba ukoo wa Temu umejaribu kujitofautisha katika kuzidi kujitambuana kutengeneza jamii yao ya pekee yao katika kuelekea kupiga hatua kubwa kimaisha kwa kila mwanaukoo bado kuna taarifa nyingi zaidi zinahitajika zinaweza kuunganisha ukoo huu na kuujengea hamasa kubwa zaidi kuelekea kutimiza yote wanayopangwa. Tunahitaji taarifa zaidi kwa ajili ya utafiti na kuongeza maudhui ya ukoo huu na koo za wachagga kwa ujumla kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Temu.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Temu?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Temu?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Temu?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Temu una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Temu wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Temu kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Temu?

9. Wanawake wa ukoo wa Temu huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Temu?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Temu?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Temu?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Temu kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *