UKOO WA SOMI.

– Somi ni ukoo wa wachagga ukiwa moja kati ya koo zinazopatikana kwa uchache sana Uchaggani, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Somi wanapatikana kwa kiasi kwenye baadhi ya vijiji katika maeneo ya magharibi ya kati ya Uchagga hususan katika eneo la Machame central lakini ukipatikana pia kwa uchache katika maeneo ya katikati ya Uchagga, Kilimanjaro.

– Huu ni ukoo mdogo lakini wenye wasomi wengi na watu watulivu. Huu ni ukoo unaoweza kuwa na mshikamano mkubwa kiukoo na kupiga hatua kwa kuwa ndugu wengi wanafahamiana kwa ukaribu na wana nafasi nzuri ya kuimarisha mahusiano baina ya wanaukoo. Ukoo wa huu ni moja kati ya koo kongwe sana za asili ya wachagga asilia Kilimanjaro.

– Ukoo huu kama tulivyouona haujasambaa sana na hivyo hautajwi sana au wengine watu wengi hawajawahi kuusikia lakini unapatikana kwenye vijiji vichache.

– Ukoo wa wa Somi unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mbosho, Masama.

– Ukoo wa Somi unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Foo, Machame.

– Ukoo wa Somi unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Korini Kati, Mbokomu, Old Moshi.

– Licha ya kwamba ukoo wa Somi ni ukoo mdogo na usio na umaarufu mkubwa lakini kuna siri nyingi sana zimejificha nyuma yake, tunahitaji kupata mchango zaidi wa mawazo kuhusu ukoo huu. Tunahitaji kuongeza maudhui zaidi kwenye maktaba ya ukoo huu na hususana kwenye koo za wachagga, Kilimanjaro kwa faida ya watu wote wenye hitaji la kufahamu undani wa koo hizi kwa manufaa mbalimbali hususan maendeleo na ustawi wa wachagga.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Somi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Somi?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Somi?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Somi?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Somi una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Somi wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Somi kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Somi?

9. Wanawake wa ukoo wa Somi huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Somi?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Somi?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Somi?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Somi kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp/Call +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *