UKOO WA MKENDA.

– Mkenda ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi katika ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye chimbuko lake zaidi katika eneo la Mashati, Rombo ambao umekuwa na watu wengi mashuhuri katika historia.

– Ukoo wa Mkenda ni ukoo wenye watu wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali kuanzia biashara na ujasiriamali, taaluma na kwenye taasisi mbalimbali za ndani ya nchi na kimataifa. Ukoo huu japo haukutoa watawala katika miaka ya zamani lakini ulihusika zaidi katika nyanja nyingine za kisiasa Uchaggani, hususan katika eneo ukanda huu wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro hususan kutoa askari wengi hodari vitani na kulinda himaya.

– Ukoo wa Mkenda umeendelea kuongezeka na kusambaa maeneo mengine zaidi na vijiji vingi zaidi vya ukanda wa mashariki ya mbalimbali ya Uchagga, Kilimanjaro na hata kusogea mpaka katika ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro.

– Hivyo ukoo wa Mkenda unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkolowony, Mamba.

– Ukoo wa Mkenda unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mboni, Mamba.

– Ukoo wa Mkenda unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Matala, Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Mkenda unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Uuwo, Mwika.

– Ukoo wa Mkenda wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mamsera Kati, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Mkenda unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Makiidi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Mkenda unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mrao, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mkenda wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mmomwe, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mkenda wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kerio, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mkenda wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Keni, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mkenda unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kirua-Rombo, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mkenda unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kiraeni, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mkenda unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mrere, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mkenda unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kisale, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mkenda unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mahorosha, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Mkenda unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Msaranga, Mashati, Rombo.

Karibu kwa mchango zaidi kuhusu ukoo wa Mkenda. Ukoo wa Mkenda ni ukoo mkubwa na una historia kubwa na ya ndani zaidi lakini mengi ya kuhusu ukoo wa Mkenda yamejificha na mengine yamepotea pia. Tunahitaji kuwa na maudhui mengi zaidi ya kuhifadhi katika maktaba ya ukoo wa Mkenda na maktaba ya wachagga kwa ujumla. Lengo la maudhui haya ni kujenga kujitambua kwa jamii ya wachagga kwa ujumla na kujenga hamasa, umoja na mshikamano miongoni mwa wachagga katika kuelekea kufanya mambo makubwa zaidi kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja na jamii yote kwa ujumla.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Mkenda.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mkenda?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mkenda?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mkenda?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mkenda una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Mkenda wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mkenda kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mkenda?

9. Wanawake wa ukoo wa Mkenda huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mkenda?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mkenda?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mkenda?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mkenda kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *