– Kisamo ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi katika eneo la mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro hususan Marangu. Huu ni ukoo wa wenye watu wengi makini na wasomi wakubwa ambao wanafanya vizuri sana katika nyanja kuanzia taaluma, biashara n.k., katika taasisi na mashariki mbalimbali ndani na nje ya nchi.
– Ukoo wa Kisamo sio ukoo mkubwa lakini umesambaa kiasi, huku ukiwa ni ukoo wenye wachagga wenye mshikamano na ushirikiano mkubwa baina yao na wakiwa wengi ni watu wenye kujitambua sana.
– Kisamo pia ni kijiji au tunaweza kusema ni usharika katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi ukiwa na kanisa la kilutheri upande wa Kaskazini wa kijiji hicho. Wachagga wenyewe wa ukoo wa Kisamo wanasema kwamba mwanzilishi wa eneo hilo la Kisamo, Old Moshi ametokea kwenye ukoo wao licha ya kwamba ukoo huu unapatikana kwa wingi zaidi Marangu kuliko katika eneo hilo la Kisamo, Old Moshi ambapo ukoo wa Kisamo unaamini makazi yake yameanzishwa na mtu kutoka katika ukoo wao.
– Ukoo huu wa Kisamo umesambaa zaidi katika eneo hili hili la mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro na kwa uchache huko mashariki ya mbali pia.
– Hivyo ukoo wa Kisamo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu.
– Ukoo wa Kisamo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Arisi, Marangu.
– Ukoowa Kisamo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyasomboro, Marangu.
– Ukoo wa Kisamo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mshiri, Marangu.
– Ukoo wa Kisamo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Ashira, Marangu.
– Ukoo wa Kisamo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Samanga, Marangu.
Ukoo wa Kisamo ni ukoo wenye wasomi wengi na watu makini. Hata hivyo bado hakuna maudhui mengi yaliyoandikwa kuhusu ukoo huu, hivyo kuna maswali mengi ambayo hayajajibiki kuhusu ukoo wa Kisamo. Tunahitaji kufahamu mengi zaidi kuhusu ukoo wa Kisamo na namna historia yake inaendana na eneo la Kisamo, Old Moshi pia ili kuhifadhi maudhui mengi zaidi katika maktaba ya ukoo huu na jamii ya wachagga kwa ujumla. Tunahitaji kuhifadhi taarifa na maudhui katika maktaba za mitandaoni na maktaba halisi pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja kujitambua na kujijengea kujiamini zaidi kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha katika ngazi ya mtu mmoja mmoja kwenye ukoo wa Kisamo, ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.
Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Kisamo.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kisamo?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kisamo?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kisamo?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kisamo una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Kisamo wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kisamo kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kisamo?
9. Wanawake wa ukoo wa Kisamo huitwaje, na kwa nini?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kisamo?
11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kisamo?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kisamo?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kisamo kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).
Whatsapp +255 754 584 270.