Katika nchi ya wachagga hadhi ya mwanamke kisheria na haki zake zilikuwa bayana na zaidi zinaonekana wakati wa ndoa. Hata hivyo mbele ya sheria za wachagga mwanamke alipewa hadhi kubwa zaidi kisheria ukilinganisha na jamii nyingi za kiafrika. Kwa mfano katika ardhi ya wachagga miaka ya zamani sana wakati wa vita kisheria mwanamke hakuruhusiwa kushambuliwa, …
Category: Makala
ADHABU ZA NCHI YA WACHAGGA ZILITOKANA NA MTU KUFANYA MAPENZI NJE YA UTARATIBU.
Binti alipoolewa halafu yule Bwana harusi akakuta kwamba binti yule alikuwa ni bikra, ilikuwa ni desturi kwamba atachinja kondoo na kuwatumia nyama wazazi wa binti huyo, ambao nao pia watatuma tena kondoo kwa binti yao kwa kumshukuru binti yao kwa viwango vya juu vya maadili alivyozingatia. Lakini ikiwa binti ameolewa na kukutwa kwamba hakuwa bikra, …
HADITHI YA WACHAGGA INAYOTOA MAONYO JUU YA MTU KUKOSA SHUKRAN KWA MATENDO MEMA ALIYOFANYIWA NA WENGINE.
Wachagga wa miaka ya zamani za kale walifahamu kwamba mtu anapofariki huenda kwenye dunia ya rohoni. Kisha mtu hubaki kwenye dunia hii ya roho mpaka pale anapofikia kuwa roho kweli. Lakini hukaa tena kwenye dunia hii ya rohoni mpaka anazeeka kisha anakwenda kwenye dunia nyingine ya ngazi ya pili ya roho ya watu waliofariki miaka …
HADITHI YA WACHAGGA INAYOONYESHA MADHARA YA MTU KUKOSA SHUKRANI KWA “RUWA”.
Hapo zamani za kale katika nchi ya wachagga kulikuwa na mwanamke ambaye hakujaliwa kabisa kupata mtoto hata mmoja. Mwanamke huyu pia umri wake wa kuweza kupata mtoto ulikuwa umepita sana. Kila siku alikuwa akifanya kazi mpaka kufikia kuchoka sana huku wanawake wengine wakimkejeli na kumsanifu kwa kutokuwa na mtoto ambaye angeweza kuwa msaada kwake. Jambo …
HADITHI ZA WACHAGGA ZINAZOONYESHA UTHABITI NA UHAKIKA WA MIPANGO YA “RUWA/IRUWA”.
Hapo zamani za kale katika nchi ya wachagga inasemekana kwamba kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa mwizi kuzidi watu wote. Siku moja mtu huyu mwizi alienda kwenye nyumba ya watu wengine usiku wa manane kwenda kuiba ulezi. Usiku huo huo mke wa huyo mwenye nyumba aliyoenda kuiba alikua amejifungua mtoto wa kike. Lakini katika nyakati hizo …
HADITHI INAYODHIHIRISHA UKUU WA “RUWA/IRUWA” KWA WACHAGGA.
Zamani katika miaka ya mwishoni mwa karne ya 18 au miaka ya 1790’s kulikuwa na watawala wawili wenye nguvu sana mashariki ya Kilimanjaro. Watawala hawa walikuwa ni Mangi Horombo wa Keni na Mangi Rongoma wa Kilema. Mangi Horombo wa Keni, Rombo akitawala kuanzia kuanzia Mriti/Mamsera mpaka Usseri na Ngasseni upande wa mashariki zaidi huku Mangi …
HADITHI YA “MORILE” KWA WACHAGGA.
Hapo zamani za kale wachagga walifahamu kwamba kulikuwa na Mungu aliyeumba watu ambaye aliishi kwenye juu huko juu mawinguni. Wachagga walijua pia kwamba Mungu huyo amewatendea watu mambo mema mengi sana. Lakini wachagga waliendelea kuliangalia anga la juu na kutamani kufahamu mambo mengi sana kuhusu anga ambalo jua hupita kila siku. Lakini hawakuweza kupata mtu …
HADITHI ZA DINI YA ASILI YA WACHAGGA KABLA YA KUJA KWA WAMISIONARI WA KIKRISTO – 5
UKUU WA RUWA/IRUWA. Tumeweza kuona kwamba hadithi ya kwanza katika mfululizo huu wa hadithi za zamani za wachagga inafanana sana na hadithi ya kwenye biblia ya anguko la kwanza la mwanadamu kwenye bustani ya Edeni. Halafu hadithi ya pili inafanana sana na hadithi ya Kaini na Habili. Kisha tumeona hadithi iliyofuata ya kuangamizwa kwa dunia …
HADITHI ZA DINI YA ASILI YA WACHAGGA KABLA YA KUJA KWA WAMISIONARI WA KIKRISTO – 4
DUNIA KUANGAMIZWA KWA MARA YA PILI. Baada ya Mkechuwa kufariki watoto wake na kizazi chake kwa ujumla kiliongezeka sana na walitajirika sana pia. Hii ilichangiwa pia na mifugo yao kupata majani mengi kwa sababu dunia bado ilikuwa haijawa na watu wengi sana. Watu matajiri walianza tena kujivuna sana na mali zao pamoja na vyakula tele …
HADITHI ZA DINI YA ASILI YA WACHAGGA KABLA YA KUJA KWA WAMISIONARI WA KIKRISTO – 3
RUWA/IRUWA AINGAMIZA DUNIA. Hapo zamani za kale watu waliendekeza uvivu na kutelekeza majukumu yao na kuwaagiza watu maskini na wanyonge kuwafanyia kazi zao. Kisha watu matajiri wakagoma kabisa kufanya kazi kwa namna yoyote ile. Walisubiri mpaka watu maskini na wenye uhitaji kuvuna mazao yao na mara baada ya kuvuna matajiri na wenye uwezo waliwapora kwa …