UKOO WA TENGA/MTENGA.

– Tenga na Mtenga ni ukoo wa mkongwe na wenye umashuhuri sana kwa baadhi ya maeneo ya Uchagga, Kilimanjaro ambao umeoyesha umahiri mkubwa katika nyanja mbalimbali katika nyakati tofauti tofauti za kihistoria. Hata hivyo japo hakuna taarifa za kutosha zinazoweza kuunganisha matawi ya ukoo huu kwa usahihi kwa maeneo yote zinakopatikana katika ardhi ya Uchagga, …

UKOO WA MANGESHO.

– Mangesho ni ukoo wa wachagga unaopatikana katika eneo la mwishoni mwa ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga na kwa kiasi katika eneo la katikati la ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Hata hivyo bado hakuna taarifa za uhakika kama ukoo wa Mangesho wa eneo hili la katikati ya ukanda wa mashariki …

UKOO WA MREMI.

– Mremi ni ukoo wa wachagga wenye umaarufu kiasi unaopatikana kwa wingi zaidi katika ukanda wa mwishoni mwa mashariki ya kati ya Uchagga na mwanzoni mwa ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Ni ukoo wenye watu mbalimbali makini wanaofanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali hasa biashara na ujasiriamali. – Kutoka kwenye historia Mremi …

UKOO WA MKENDA.

– Mkenda ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi katika ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye chimbuko lake zaidi katika eneo la Mashati, Rombo ambao umekuwa na watu wengi mashuhuri katika historia. – Ukoo wa Mkenda ni ukoo wenye watu wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali kuanzia biashara na …

Mfahamu ELIFURAHA NDESAMBURO URIO MAREALLE.

– Elifuraha alizaliwa huko Mwika, Moshi, Kilimanjaro mwaka 1929. – Alisoma katika shule ya Sekondari ya wasichana Ashira ambapo baadaye alikuja pia kufundisha tena kama mwalimu katika shule hiyo. – Mwaka 1955 Elifuraha alikuwa mmoja kati ya wanawake watatu wa kwanza kuwa wabunge Tanganyika, yeye peke yake akiwa ndiye mwafrika. Hivyo ni mwanamke wa kwanza …

Habari Ndugu Wana-Urithi Wetu Wachagga.

Leo Tunafunga Mwaka 2023 na Kwenda Kuuanza Mwaka Mpya wa 2024. Kwa Muda Mrefu Tumekuwa Tunaweka Hapa Makala Mbalimbali za Kuelimisha na Nyingine za Kuburudisha. Leo Kabla Ya Kuufunga Mwaka Huu wa 2023 Tungependa Kupata Mrejesho na Maoni Yako Juu Ya Mambo Mbalimbali. 1. Nini Kikubwa Ulichojifunza Ambacho Hukuwa Unafahamu Kabla? 2. Nini Kilikuvutia Zaidi …

UCHAMBUZI WA KITABU. – SEHEMU YA 11.

*Maisha Ya Mchagga Hapa Duniani Na Ahera” By Mangi Petro Itosi Marealle* Uchambuzi by Mary Assenga. USAWI (UCHAWI) KWA WACHAGGA. -Katika nchi ya Uchagga tuliogopa sana “usawi” (uchawi) toka zamani sana. Huu uchawi ulitisha watu wote, wakubwa kwa wadogo, waume kwa wake, watoto mpaka Wamangi. Ulitisha kuliko magonjwa ya kifua kikuu na ndui. Kwani mtu …

UCHAMBUZI WA KITABU. – SEHEMU YA 10.

*Maisha Ya Mchagga Hapa Duniani Na Ahera” By Mangi Petro Itosi Marealle* Uchambuzi by Mary Assenga. “MIZIMU” -Wachagga zamani waliamini na kutambikia mizimu, yaani watu wao walio marehemu. Waliamini mtu akishakufa bado alikwenda kuishi tena kule kuzimuni, lakini si kwa mwili huu tulio nao. Wachagga walisadiki kuwa hawa mizimu hula na kunywa, na kuweza kuja …

UCHAMBUZI WA KITABU. – SEHEMU YA 9.

*Maisha Ya Mchagga Hapa Duniani Na Ahera” By Mangi Petro Itosi Marealle* Uchambuzi by Mary Assenga. IMANI YA WACHAGGA. “RUWA” -Wachagga huamini “Ruwa”(Mungu) kwamba ni Mkuu kupita mizimu yote wanayotambikia. Huyu Ruwa hasumbui wanadamu kwa sababu ndogondogo kama vile mizimu iwasumbuavyo ikiwa haikutambikiwa. Tambiko alilotolewa Ruwa ni tofauti na tambiko la mizimu kwa hali na …