ASILI YA MUNGU “RUWA/IRUWA” WA WACHAGGA.

ASILI YA MUNGU “RUWA/IRUWA” WA WACHAGGA.

Inafahamika Wazi Kwamba Zamani Kabla Ya Kuja Kwa Dini Kubwa Kubwa Duniani Kila Jamii Ilikuwa na Dini Yao Na Mungu Wao wa Peke Yao. Ndio Maana Hata Kwenye Biblia Takatifu Katika Kitabu cha Kutoka 20, Katika Amri Kumi za Musa Amri Ya Kwanza Inasema, “Mimi ni Bwana Mungu Wako, Usiabudu Miungu Mingine Ila Mimi”. Amri Hii Inasema Hivi Kwa Sababu Zamani Kulikuwa na Miungu Wengi. Na Sio Tu Kwamba Kila Jamii Ilikuwa na Mungu Wake Bali Kuna Jamii Nyingi za Kale Zilizokuwa na Dhana Ya Kundi La Miungu(Polytheism), Ambalo Liko Chini Ya Mungu Mmoja Mkuu Ambapo Kila Kitu Kwenye Maisha Kilikuwa na Mungu Wake Maalaumu Anayeshughulika Nacho Katika Kundi Hilo La Miungu, Huku Mungu Mkuu Akiwa Ndiye Mwamuzi wa Mwisho.

Wamisri wa Kale Walikuwa na Mungu Wao Mkuu Aliyeitwa Amun-Ra, Waasiria Waliokuja Kuitawala Babeli Ya Kale Walikuwa na Mungu Wao Mkuu Aliyeitwa Ashur, Waajemi Walikuwa na Mungu Wao Mkuu Aliyeitwa Ahura Mazda Kupitia Dini Yao Ya “Zoroastrianism” Wayunani wa Kale Walikuwa na Mungu Wao Mkuu Aliyeitwa Zeus, Warumi wa Kale Walikuwa na Mungu Wao Mkuu Aliyeitwa Jupita. Wayahudi Nao Mungu Wao Aliitwa Yehova Ambaye Ndiye Baadaye Alikuja Kuwa Mungu wa Wakristo Pia.

Yaani Kila Jamii Zamani Ilikuwa na Mungu Wake na Hakukuwa na Injili za Kuwashawishi Watu Wote Kuwa Chini Ya Mungu Mmoja, Kila Mtu Alikuwa na Mungu Wake na Ilionekana ni Kawaida Japo Wakati Mwingine Kulikuwa na Mashindano Ya Mungu Gani Mwenye Nguvu Zaidi Ya Mungu wa Wengine na Hilo Lilionekana Katika Kuonyeshana Ubabe Kwenye Vita na Mambo Mengine. Ndio Maana Utaona Hata Katika Biblia Inaonekano Mungu wa Musa Akijaribu Kushindana na Mungu wa Farao wa Misri Ya Kale Kujaribu Kuonyeshana Yupi Mwenye Nguvu Zaidi, Au Kipindi Wayahudi Wanapambana na Wafilisti na Mungu wa Wayahudi Kuwaahidi Ushindi Dhidi Ya Mungu wa Wafilisti. Hayo Yalikuwa Ni Mashindano Ya Mara Kwa Mara Ya Miungu Lakini Hakukuwa na Injili Ya Kuwashawishi Watu Kuwa Chini Ya Mungu Mmoja Kwa Nyakati Hizo.

Ni Baadaye Miaka 300 AD Ndipo Mtawala Constantine wa Rumi Ya Kale Alipoamua Kwamba Ukristo Utakuwa Dini Rasmi Ya Himaya Ya Rumi Ndipo Mambo Yalipoanza Kubadilika Ambapo Ukristo Kupitia Himaya Ya Rumi Ulianza Kusambazwa Kwa Kasi na Wakati Mwingine Kwa Lazima Kwenye Maeneo Yote Ya Utawala na Makoloni Ya Rumi Ya Kale. Mwaka 529 AD Mtawala Justinian wa Himaya Ya Rumi Ya Kale Ya Mashariki Maarufu Kama “Byzantine Empire” Alipopiga Marufuku Falsafa Nyingine Zote na Dini Zote Katika Himaya Yote Ya Rumi Ya Kale na Makoloni Yake Yaliyokuwa Yameenea Ulaya Yote, Baadhi Ya Maeneo Ya Mashariki Ya Kati, Kaskazini Ya Afrika na Magharibi Ya Asia na Badala Yake Kuenezwa Kwa Falsafa Ya Kanisa Katoliki Peke Yake. Hapo Ndipo Dhana Ya Kuwa na Mungu Mmoja Kwa Mataifa Mengi Ilienea na Kusambaa Eneo Kubwa Sana na Kugeuka Kuwa Ndio Utamaduni.

SASA NI IPI ASILI YA MUNGU “RUWA” WA WACHAGGA?

Kwanza Tunafahamu Kwamba Wachagga Asili Kabla Ya Kuteremka Kuelekea Kusini Ya Afrika Walitokea Maeneo Ya Kusini Ya Misri Mnamo Karne Ya 13 au 14. Eneo Hili La Kusini Ya Misri Ambalo Lipo Nje Ya Ile Himaya Kuu Ya Misri Ya Kale, Mungu Aliyekuwa Anaabudiwa Aliitwa Mungu “Ra” Ambayo Kwa Lugha Ya KiMisri Ya Kale Ilitamkika “Rhuwa”.

Mungu Ra(Rhuwa) Kwa Namna Inavyotamkwa Kwa Lugha Ya Misri Ya Kale, Lugha Ambayo Ilishakufa Katika Matumizi Aliaminiwa Kwamba Ndiye Mungu Mtawala wa Dunia Yote Iliyoumbwa Yaani Anga, Dunia na Chini Ya Dunia na Bahari. Mungu Ra(Rhuwa) Kama Inavyotamkwa Kwa Lugha Ya Misri Ya Kale Pia Aliaminiwa Kuwa Ndiye Mungu wa Jua, Mpangilio wa Vitu Katika Ulimwengu, Wafalme na Anga.

Mungu Ra(Rhuwa) Alikuwa Ndiye Mungu Aliyekuwa Anaaminiwa Katika Misri Ya Kale Tangu Miaka 4,500 Iliyopita Lakini Miaka 500 Baadaye Ikaibuka Dhana Nyingine Ya Mungu Amun Ambaye Mara Nyingi Aliunganishwa na Mungu Ra(Rhuwa) na Kuitwa Amun-Ra(Rhuwa). Baadaye Miaka 3350 Iliyopita Wakati wa Farao Akhenaten wa Kizazi cha 18 cha Mafarao wa Misiri Ya Kale Alijaribu Kurudisha Dhana Ya Imani Ya Mungu Ra(Rhuwa) Lakini Akiwa Amefanya Mabadiliko Ya Namna Ya Umungu Wenyewe Kwa Namna Ya Kujitukuza Zaidi Yeye Binafsi Akiita Aten Lakini Baada Ya Kifo Chake Ilitelekezwa na Watu Kwenye Imani Ya Amu-Ra.

Imani Ya Mungu Ra(Rhuwa) Ilikuwa Kubwa na Muhimu Kwa Miaka Mingi Sana Lakini Sio Mabadiliko Yote Yaliyokuwa Yanatokea Katika Nyakati Tofauti Tofauti Yaliendelea Kufikia Kila Eneo. Hivyo Tamaduni za Kuamini Katika Mungu Ra(Rhuwa) Zilizoenea Sana Katika Maeneo Hayo Ya Himaya Ya Misri Ya Kale na Zilizodumu Kwa Maelfu Ya Miaka Kabla Ya Kuanza Kupotea Taratibu Baadaye Kutokana na Kuingizwa Kwa Imani Nyingine Zilizotokea Upande wa Pili wa Bahari Ya Mediterranean Ndizo Wachagga Walizokuwa Nazo na Walizoendelea Kubaki Nazo.

Wachagga Asili Walipohama na Kuteremka Kuelekea Kusini Karne Ya 12 au 13 Waliondoka na Imani Hiyo Hiyo Ya Kuamini Katika “Rhuwa” na Walipokuja Kuingia Kilimanjaro Baadaye, Bado Mungu Aliendelea Kubaki Kuwa ni “Ruwa” na Waliamini Mlima Kilimanjaro Ndio Makazi Ya Ruwa na Ndiye Aliyewaongoza Kufika Kilimanjaro na Wakamshukuru Sana Kwa Kumtolea Sadaka. Licha Ya Kwamba Kuna Makabila Ya Pembeni Ya Kilimanjaro Hususan Wataita, Wakamba, Wamasai, Wakwavi na Wataveta Ambao Walikuwa Wanaabudu Katika Miungu Mingine Hususan “Ngai(Mungu wa Wakamba, Wamasai na Wakikuyu)” Ambao Walijipenyeza na Kuingia Kuchanganyika na Wachagga Asili Kilimanjaro Kwa Kiasi, Lakini Bado Mungu wa Wachagga Aliendelea Kubaki Kuwa Ni Ruwa.

Mungu “Ruwa” Alikuwa na Nguvu Sana Kwa Wachagga na Hata Hadithi Nyingi za Kale za Wachagga “Chagga Legend Stories” Kiini Chake Ni “Ruwa” na Ndio Maana Hata Licha Ya Mwingiliano Kiasi na Jamii za Pembeni Ya Kilimanjaro Bado Mungu Wa Wachagga Aliendelea Kubaki Kuwa ni “Ruwa”.

Wamisionari wa Kikristo Waliokuja Kueneza Injili Ya Kikristo Kwa Wachagga Karne Ya 19 Walikuja Kueneza Habari za Kristo Ambaye Alitoka Kwa Mungu Yehova Aliyekuwa Mungu wa Wayahudi Zamani. Lakini Ili Kupata Urahisi wa Kueleweka na Wachagga Ilibidi Wawaaminishe Wachagga Kwamba “Ruwa” Ndiye Yehova. Pengine Wamisionari wa Kikristo Waliamua Kufanya Hivi Kwa Sababu Kulikuwa na Ufanano Mkubwa Kati Ya “Ruwa” na Yehova na Kisha Kuanza Kuwafafanulia Zaidi Wachagga Habari za Yehova Ambazo Ni Nyingi Zaidi na Nyingine Zikitofautiana Kidogo na Zile za Ruwa Wanazozifahamu.

Hata Hivyo Kuna Hadithi Nyingi za Kwenye Biblia(Legend Stories) Hususan Agano La Kale Ambazo Zina Ufanano Mkubwa na Hadithi Nyingi za Kwenye Dini Ya Wachagga Ya Zamani Ambayo Kiini Chake Ni “Ruwa” Kama Vile Hadithi Ya Gharika Ya Nuhu, Hadithi Ya Kula Tunda Kwenye Bustani Ya Edeni, Hadithi Ya Esau na Yakobo Kuhusu Haki Ya Uzaliwa wa Kwanza n.k. Pengine Hii Iliwasukuma Wamisionari Kumhusisha Yehova na Ruwa na Ufanano wa Hadithi za Kwenye Biblia na Hadithi za Dini Ya Wachagga Ya Zamani Zikarahisisha Wachagga Wengi Kuuelewa na Kuukubali Ukristo.

Ahsanteni.

Karibu kwa Maswali, Maoni au Nyongeza.

ASILI YA MUNGU “RUWA” WA WACHAGGA
ASILI YA MUNGU “RUWA” WA WACHAGGA
ASILI YA MUNGU “RUWA” WA WACHAGGA
ASILI YA MUNGU “RUWA” WA WACHAGGA
ASILI YA MUNGU “RUWA” WA WACHAGGA

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *