LUGHA YA WACHAGGA NI MOJA.

LUGHA YA WACHAGGA NI MOJA.

– Kumekuwa na Utata wa Muda Mrefu Kuhusu Kama Wachagga Wanaongea Lugha Moja Au Ni Lugha Mbalimbali Tofauti, Jambo Ambalo Limeleta Utata Mwingine wa Kwamba Kama, Je Wachagga Ni Jamii Moja Au Ni Jamii Mbalimbali Zilizojikuta Zinaishi Kwenye Mlima Kilimanjaro na Kuamua Kujiita Kwa Pamoja Wachagga?

– Jibu Ni Lugha Ya Kichagga ni Moja, Lakini Ikiwa Katika Lahaja Mbalimbali za Kichagga. Wachagga Ni Jamii Moja Iliyogawanyika Katika Himaya Mbalimbali na Lahaja Mbalimbali Za Lugha Moja Kuu Ya Kichagga.

– Swali Lingine ni Je, Kwa Nini Kuwe na Lahaja Mbalimbali Kusiwe na Lugha Moja Tu Ya Kichagga Kama Ni Jamii Moja?

– Tunasema Kichagga ni Lugha Moja kwa Sababu Mwanzoni Kabisa Kulikuwa na Lugha Moja Ya Kichagga Inayofanana kwa Kila Kitu Ambayo Ilikuwa Inazungumzwa na Wachagga Wote Kilimanjaro Wakati Wachagga Wanahamia Kilimanjaro Wakiwa Kama Jamii Moja.

– Baada Ya Kuishi Kilimanjaro kwa Muda, Watu wa Jamii Nyingine Kutoka Nje Ya Kilimanjaro Walianza Kuhamia Kilimanjaro kwa Kasi Kuungana na Wachagga Waliokuwa Wanaishi Kilimanjaro. Watu Hawa Waliotokea Pande Mbalimbali za Kilimanjaro Ambao Waliingia kwa Makundi Madogo Madogo Ndio Walisababisha Lugha Halisi Ya Wachagga Kuendeleza Utofauti Uliotokea Kati Ya Eneo Moja na Jingine Kwa Sababu Walikuwa Wengi Kiasi.

– Wingi wa Watu Waliohamia Kilimanjaro Kuungana na Wachagga Walitokea Upande wa Mashariki Ambao Kwa Sehemu Kubwa Leo Hii Ni Nchi Ya Kenya Ambapo Zaidi Walitokea Jamii za Wataita na Wakamba na Wamasai Pia. Eneo Lilioathirika Zaidi na Mwingiliano Huu Kuliko Maeneo Mengine Yote ni Eneo La Rombo, Hasa Upande wa Mashariki Zaidi. Lakini Hata Upande wa Magharibi wa Uchagga Waliingia Kiasi Wamasai Lakini Sio kwa Wingi Kama Mashariki.

– Kwanza Inajulikana Kwamba Eneo La Katikati Ya Uchagga Kuanzia Uru, Old Moshi na Vunjo Yote(Maarufu Kama Marangu) Mpaka Mwika Wanaongea Lugha Moja kwa Karibu Asilimia 100%, Huku Eneo La Vunjo Peke Yake Wakiongea Lugha Moja kwa Asilimia 100%, Huku Kibosho Nayo Lugha Ikiendana na Eneo Hili La Katikati Ya Uchagga kwa Zaidi Ya 80%, na Hata Karibia Nusu Ya Rombo Kuanzia Mamsera Mpaka Mkuu Lugha Ikikaribiana Sana na Hili Eneo La Katikati Ya Uchagga.

– Upande wa Magharibi Kabisa na Upande wa Mashariki Kabisa Ndio Lugha Inakaribiana Kwa Asilimia Kama 60% – 70% Peke Yake, Lakini Bado Ukifuatilia Vizuri Utakuta Aidha Asili Ya Maneno Mengi Ni Yale Yale, Au Utakuta Kuna Maneno Mbadala Ambayo Yanafanana Au Yanakaribia Kufanana Na Ya Hili Eneo La Katikati Ya Uchagga.

– Kwa Mfano, Neno “Nyumbani” Kwa Wachagga wa Hili Eneo La Katikati Wanasema “Kanyi”, Ukienda Machame Japo Nyumbani Imezoeleka Kama “Boo” Lakini Neno Lingine Mbadala La Tafsiri Ya “Nyumbani” Ni “Kenyi” Ambalo Linafanana Tena Kidogo na Neno “Kanyi” Linalotumiwa na Wachagga Wa Eneo La Katikati Kumaanisha Nyumbani.

– Mfano Mwingine Ni Neno “Chakula” Ambalo Kwa Wachagga wa Hili Eneo La Katikati Wanaita “Kyelya”, Ukienda Machame Japo Chakula Wanaita “Shonga”, Lakini Wakisikia Kyelya Wanaelewa Ni Chakula.

– Hivyo Tunasema Kwamba Lugha Ni Moja Kwa Sababu Kwa Sehemu Kubwa Inafanana, na Kwa Yale Maeneo Yenye Utofauti Utakuta Aidha Ni Utofauti Wa Utamkaji, Au Kuna Msamiati Mbadala Unaoendana na Kichagga cha Eneo La Katikati, Au Kuna Msamiati Ulishasahaulika Zamani Uliokuwa Unaendana na Kichagga cha Eneo Katikati Ya Uchagga. Hivyo Inabaki Kwamba Asili Ya Lugha Ni Moja na Huo Mgawanyiko Ni Lahaja Tu Za Lugha Kuu Moja Ya Kichagga.

Suala La Jamii Moja Kuwa na Lahaja Nyingi za Lugha Kuu(Dialects) Sio Jambo La Ajabu Au Jambo La Wachagga Peke Yao. Hili Tunaweza Kuliona Pia kwa Uyunani Ya Kale Ambao Walikuwa Ni Jamii Moja Lakini Iliyogawanyika Kama Walivyo Wachagga Ambapo Kulikuwa na Wayunani wa Athene, Wayunani wa Spata, Wayunani wa Korintho, Wayunani wa Thebe, Wayunani wa Sirakusa, Wayunani wa Makedonia, Wayunani wa Egina, Wayunani wa Rodo, Wayunani wa Eretria n.k.,.

– Wote Hawa Walikuwa Ni Jamii Moja Ya Wayunani Lakini Waliokuwa Wamegawanyika Katika Himaya Ndogo Ndogo Nyingi na Licha Ya Kwamba Walikuwa na Lugha Moja Ya Kiyunani Lakini Ilikuwa Katika Lahaja Mbalimbali za Kiyunani.Wayunani Walikuwa Ni Wasomi, Wanasayansi, Wanafalsafa, Watawala, Wafalme Wakuu na Watu Mashuhuri Sana wa Dunia Ya Kale, Hata Licha Ya Kwamba Harakati za Dini Ya Kikristo Zilianzishwa na Watu wa Asili Ya Kiyahudi Lakini Biblia Ya Kwanza kwa Upande wa Agano Jipya Iliandikwa kwa Kiyunani cha Lahaja Ya “Koine” Kwa Sababu Ndio Iliyokuwa Lugha Ya Wasomi na Watu Mashuhuri kwa Nyakati Hizo, Ambapo Hata Alexander Mashuhuri(Alexander the Great) Alikuwa ni Myunani, Wakati Huo Wayahudi Wakiwa ni Watu wa Hadhi Ya Chini Ambao Hata Lugha Yao Haikuwa Imejitosheleza Sana Kimaandishi na Isiyo na Heshima Kubwa.

– Hata Biblia Ya Kwanza Ya Agano La Kale Ya Kiyahudi “Septuagint” Iliyoandikwa Kwa Ajili Ya Wayahudi(Waisrael) Wakiwa Uhamishoni Misri Nyakati za Ptolemi Iliandikwa Kwa Kiyunani cha Lahaja Ya Koine.

– Hivyo Lugha Kuu Ilibaki Kuwa ni Kiyunani Lakini cha Lahaja Fulani, na Sio Lahaja Kugeuka Kuwa Lugha Kuu.

– Kwa Mujibu wa Mary Kathleen Stahl, Mmoja Kati Ya Wanahistoria Maarufu wa Kichagga, Kutokana na Mapinduzi na Mabadiliko Makubwa Ya Kisiasa Yaliyokuwa Yanaendelea kwa Wachagga Karne Ya 20, Lugha Ya Kichagga Ilikuwa Imeanza Kubadilika Taratibu Kuelekea Kuwa Moja Tena na Endapo Mwenendo wa Mambo Ungeendelea Vile Vile Kama Ulivyokuwa Unaenda Kabla Ya Uhuru wa Tanganyika Wachagga Wangerudi Tena Kwenye Lugha “Standard” Moja Ndani Ya Kipindi cha Miaka 30 Mpaka 50.

– Mangi Mkuu wa Wachagga Thomas Lenana Marealle Alitaka Kuharakisha Zoezi Hili kwa Kurasimisha Lugha Ya Kichagga Miaka Ya 1950’s, na Kwa Kuanza Alitaka Magazeti Ya Wachagga Yaandikwe kwa Lugha Ya Kichagga na Lugha Ya Kichagga Iendelee Kutumika Baadhi Ya Maeneo Kama Lugha Rasmi, Kama Walivyofanya Kanisa La Kilutheri. Hata Hivyo Mangi Mkuu Alikutana na Changamoto Kiasi Kutokana na Kutokuwa na Sauti Ya Mwisho na Hivyo Utekelezaji Wake Ukafifia Kidogo Miaka Ya Kabla Ya Uhuru wa Tanganyika.

Karibu kwa Maoni, Ushauri, Nyongeza au Mawazo Mbadala.

LUGHA YA WACHAGGA NI MOJA
LUGHA YA WACHAGGA NI MOJA

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *