UKOO WA MASAKI.

– Ukoo wa Masaki ni ukoo maarufu katika eneo la himaya ya umangi Siha/Sanya Juu katika vijiji vya Samaki Maini na Mae. Wachagga wa ukoo wa Masaki wakiwa wameshuka kutoka kwenye plango ya Shira waliweka makazi yao ya mwanzoni ya kudumu katika kijiji cha Samaki Maini sambamba na ukoo wa Orio/Urio na Kileo. – Kutoka …

UKOO WA MWANDRI.

– Ukoo wa Mwandri ni ukoo mkongwe sana na maarufu katika eneo la Siha Sanya Juu. Huu ni ukoo ambao uliweka makazi yake ya kudumu katika kijiji cha Wanri, Siha upande wa juu wa hospitali ya Kibong’oto. Kijji hiki cha Wanri miaka ya baadaye kilikuja kuwa maarufu zaidi na muhimu zaidi kwenye masuala ya utawala …

UKOO WA NATAI

– Ukoo wa Natai ni ukoo mkongwe pia na mashuhuri sana upande wa Magharibi ya Kilimanjaro. Huu ni ukoo ambao unapatikana kwa wingi zaidi katika eneo la Masama magharibi katika vijiji vya Lukani, Mashua, Nkwansira, Ng’uni, Kyuu, Losaa n.k. Ukoo wa Natai wanapatikana kwa wingi pia katika vijiji vya himaya ya umangi Sanya Juu. – …

UKOO WA MUNUO.

– Ukoo wa Munuo ni ukoo mkubwa na mashuhuri sana upande wa magharibi ya mbali ya Uchaggani Kilimanjaro. Ukoo huu unapatikana katika maeneo ya Masama Magharibi hususan katika vijiji vya Lukani, Ng’uni, Kyuu, Mashua, Nkwansira, Losaa n.k. Ukoo huu unapatikana pia kwa kiasi maeneo ya Sanya Juu. – Kutoka kwenye historia ukoo wa Munuo unafahamika …

UKOO WA NKINI.

– Ukoo wa Nkini ni moja kati ya koo kongwe kabisa na mashuhuri sana katika eneo la Siha/Sanya Juu. Ukoo wa Nkini sambamba na koo nyingine katika eneo hilo walishuka kutoka kwenye plango ya Shira(Shira Plateau) na kuweka makazi yao katika vijiji vya ukanda wa juu wa himaya ya umangi Siha/Sanya Juu hususan kijiji cha …

UKOO WA MMARI.

UKOO WA MMARI. – Ukoo wa Mmari ukoo mkubwa wenye historia kubwa na uliotoa watu mashuhuri katika historia ya wachagga. Kutoka kwenye historia ukoo wa Mmari huenda chimbuko lake kwa uchaggani ni Siha/Sanya ambapo wanapatikana kwa wingi sana na umewahi kuwa ukoo wenye nguvu na uliotoa watawala imara sana wa himaya ya umangi Siha/Sanya Juu. …

UKOO WA URIO/ORIO.

– Ukoo wa Urio/Orio ni kati ya koo kubwa, kongwe na maarufu sana miongoni mwa wachagga. Kwa uchaggani ukoo wa Urio/Orio unaaminika kwamba ulianzia Sanya Juu na uliweza kutoa watu mashuhuri katika historia kama Mzee Msanya ambaye anasemekana alihamia Meru kwa muda na kisha kurudi Sanya Juu na baadaye vizazi vyake kusambaa maeneo mengine ya …

MZEE WA MWISHO ALIYEBAKI.

MZEE WA MWISHO ALIYEBAKI. – Mzee Pauli Shirima maarufu kama Mzee Lekramu mwenye umri wa miaka 95 anaishi katika kijiji cha Ngaseni, Usseri, Rombo. Mzee huyu Pauli Shirima akiwa na mke wake Masilayo ndiye Mzee wa mwisho uchaggani aliyebaki ambaye anaweza kuongea lugha ya Kingassa kwa ufasaha. Mzee Lekramu anaongea lugha tatu kwa ufasaha kabisa …