UKOO WA NGUMA.

– Nguma ni ukoo wa kichagga unaopatikana kwa wingi katika vijiji kadhaa vya Uchagga, Kilimanjaro maeneo ya kati mashariki. Huu ni ukoo wenye watu waliosambaa katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania wakijihusisha na shughuli mbalimbali za maofisini, biashara na ujasiriamali.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Nguma ndio ukoo uliokuwa mashuhuri zaidi na unaotawala katika kijiji cha Makami Juu, Kilema. Ukoo wa Nguma ulikuwa ukitoa watawala katika kijiji cha Makami Juu, KIlema takriban miaka 400 iliyopita sasa na baada ya utawala wa umangi kuwa na nguvu zaidi ukoo Nguma waliendelea kutoa wasaidizi wa utawala Kilema katika kijiji cha hiki kama vile wachili n.k.,

– Ukoo wa Nguma umeendelea kusambaa na unapatikana katika maeneo mbalimbali ya Uchagga hususan katika eneo la Vunjo hasa himaya za Kilema na Marangu.

– Hivyo ukoo wa Nguma umesambaa na unapatikana kuanzia katika kijiji cha Kyou, Kilema kwa kiasi.

– Ukoo wa Nguma unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.

– Ukoo wa Nguma unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Ruwa, Kilema.

– Ukoo wa Nguma unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Makami-Chini, Kilema.

– Ukoo wa Nguma unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Makami Juu, Kilema.

– Ukoo wa Nguma unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kimaroroni, Kilema.

– Ukoo wa Nguma unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Nduweni, Marangu.

– Ukoo wa Nguma unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Komalyangoe, Marangu.

– Ukoo wa Nguma unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Komela, Marangu.

– Ukoo wa Nguma unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mmbahe, Marangu.

– Ukoo wa Nguma unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Rauya, Marangu.

Ukoo wa Nguma ni kati ya koo zinazokumbukwa vizuri na historia ya wachagga lakini bado kuna uhaba mkubwa wa taarifa juu ya ukoo huu. Hivyo tunahitaji kupata taarifa zaidi kutoka kwa wahusika na wengine wenye uelewa juu ya ukoo huu. Taarifa hizi zitachangia katika tafiti zinazoendelea na zitasaidia sana katika kuongeza maudhui ya ukoo wa Nguma na koo za wachagga kwa ujumla. Hili litasaidia katika kujenga hamasa inayochochea umoja na mshikamano zaidi kuelekea kufanya makubwa katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, ukoo na hata jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Nguma.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Nguma?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Nguma?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Nguma?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Nguma una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Nguma wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Nguma kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Nguma?

9. Wanawake wa ukoo wa Nguma huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Nguma?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Nguma?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Nguma?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Nguma kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp/Call +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *