– Ukoo wa Ndossa ni ukoo wa Wachagga wanaopatikana upande wa magharibi ya Kilimanjaro. Huu ni ukoo mkubwa kiasi Machame ya magharibi na mashariki ukiwa na ngome yake katika kijiji cha Saawe, Masama.
– Watu wengi wamekuwa wakiamini kwamba kuna uwezekano wa kuwepo kwa uhusiano kati ya ukoo huu wa Ndossa na ukoo wa Ndosi unaopatikana kwa wingi katika kijiji cha Mbwoeera. Hata hivyo bado hatuna taarifa za kutosha sana juu ya chimbuko la ukoo wa Ndossa na kama una uhusiano au ni tawi la ukoo wa Ndosi. Hata hivyo ukoo wa Ndossa ni ukoo unaopatikana kwa wingi kiasi pia.
– Wachagga wa ukoo wa Ndossa wanapatikana zaidi maeneo ya katikati ya himaya ya umangi Machame yaani kati ya mto Kikafu, mto Marire na mto Namwi. Tunahitaji kufahamu zaidi kuhusu ukoo huu wa Ndossa na historia yake ya nyuma, hivyo tunahitaji ushirikiano zao wa taarifa.
– Wachagga wa ukoo wa Ndossa wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Saawe, Masama kilichopo upande wa magharibi wa mto Marire.
– Ukoo wa Ndossa wanapatikana kwa wingi kiasi pia katika kijiji cha Shari/Uraa, Machame upande wa mashariki wa mto Marire.
– Ukoo wa Ndossa wanapatikana pia katika kijiji cha Uswaa, Machame kilichopo upande wa Kusini wa kijiji cha Shari/Uraa.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Ndossa?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Ndossa?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Ndossa?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Ndossa una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Ndossa wa kutokea kijiji gani?
5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Ndossa kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Ndossa?
7. Wanawake wa ukoo wa Ndossa huitwaje?
8. Una rafiki yako yeyote wa ukoo wa Ndossa?
9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Ndossa?
Karibu kwa Maoni na Maswali.
Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.
Whatsapp +255 754 584 270